Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
KAMPUNI ya Mawasiliano hapa nchini, Yas ni miongoni mwa Kampuni zitakazotoa huduma katika Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam.
Yas na Mixx by Yas ni mshirika rasmi na mtoa huduma wa kipekee wa mawasiliano na teknolojia ya kisasa kwa wafanyabiashara wote wanaohudumiwa na kituo hicho.
Kituo hicho kilifunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Agosti 1,mwaka huu, ambapo kitakuwa na maduka zaidi ya 2,000.

Aidha, kituo hicho cha kimataifa kilianza kujengwa kati ya mwaka mwaka 2022.
“Yas tunafurahia kuwa sehemu ya mradi huu wa kimkakati unaowapa fursa wafanyabiashara kukuza uchumi wa kidijitali,”.
Katika hafla ya ufunguzi wa kituo hicho, Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas, Pierre Canton Bacara, alipata mafasi ya kukutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo.
Mara baada ya kufungua kitua hicho, Rais Samia Suluhu Hassan aliwahimiza vijana kote nchini kutumia fursa za ajira zinazotolewa badala ya kulaumu kwamba Serikali haiwaoni.

“Tunaposema Serikali tunatengeneza mazingira kwa vijana, haya ndiyo mazingira yenyewe.
“Sasa ni nyinyi kutumia hizi fursa, kutumia kama mnavyoonyesha hapa, kutengeneza vitu tuwauzie nje. Msitulaumu Serikali hatuoni; kuona kwenyewe ndiyo hivi.
“Serikali haiwezi kuja kwa mmoja mmoja ikampa hivi, lakini tumetengeneza mazingira, myatumie,” amesema Rais Samia.

More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi