January 17, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Yanga yatangulia hatua ya nne ASFC

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

BAADA ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) jana kutangaza kuishusha madaraja mawili sambamba na matokeo ya michezo yake yote yatafutwa timu ya Singida United, sasa ni rasmi kuwa klabu ya Yanga imekuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya nne ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam ‘Azam Sports Federation Cup (ASFC)’

Sababu ya timu hiyo kushushwa Daraja ni kushindwa kutokea uwanjani katika mchezo wao namba 38 wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya Alliance FC ya Jijini Mwanza ambapo adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 29:1(1.1,1.2) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Kutofika Uwanjani.

Kufuatia adhabu hiyo, Shirikisho la Soka nchini (TFF), leo limeweka wazi kuwa, mchezo huo wa Shirikisho namba 65 kati ya Yanga na Singida United uliopangwa kuchezwa Januari 5, 2020 hautakuwepo, hivyo sasa watasubiri kucheza raundi ya nne 2021.