*Mpaka sasa yafikisha Sh milioni 85 za goli la Mama
*Wamshukuru Rais Samia kwa moyo wake
Na Mwandishi Wetu, Timesmajiraonline, ZanzibarÂ
KLABU ya Yanga, imeendelea kutembelea upepo mzuri wa kuvuna mamilioni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya juzi usiku visiwani Zanzibar, kuwafunga goli 6 timu ya CBE ya nchini Ethiopia, hivyo wawakilishi hao wa Tanzania, kupata Sh Milioni 30 za Rais Samia, kama sehemu ya motisha ya ushindi wao.
Kwa ushindi huo, Yanga imefanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2024/2025, ikiwa ni mwendelezo mzuri katika michuano ya Kimataifa kwa Yanga, ambapo pia kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Ethiopia, waliibuka na ushindi wa bao 1-0, hivyo kuvuna sh milioni 5 za goli la Mama.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo, Rais wa Yanga, Engineer Hers Said, alisema motisha ya Rais Samia inachangia kwa kiasi kikubwa timu yao kupata mafanikio makubwa katika michuano ya Kimataifa.
Alisema tangu Rais Samia aanze kuonyesha upendo kwa vilabu vya Tanzania, timu yao imekuwa ikitumia mwanya huo kuhakikisha kwamba Yanga wanatamba katika michuano ya Kimataifa, wakiamini kuwa goli la mama ni maalum kwa kuwapa wachezaji wao moyo wa kufia uwanjani kama sehemu ya kukuza mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania.
“Upendo huu ni mkubwa kwa Rais wetu, hivyo tunamshukuru mama Samia kwa kutuweka pazuri ndani na nje nchi, ndio maana tunashinda kwa goli nyingi uwanjani kwa sababu wachezaji wanafahamu shauku ya Rais wetu ni kuona timu inashinda na kupata mafanikio makubwa.
“Hata ukiangalia wachezaji wanapokuwa uwanjani, utagundua nguvu zao nyingi zinachagizwa pia na mamilioni ya Rais Samia, kwetu Yanga tunamshukuru kwa kuonyesha upendo dhidi ya timu yetu,” Alisema Said.
Tangu Rais Samia aanzishe motisha ya Goli la Mama, Yanga wameonyesha shauku kubwa ya kupata fedha hizo, ambapo kwa msimu huu tu tayari wamevuna Sh milioni 85 za Goli la Mama.
Mwisho
More Stories
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya