January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Yanga yaanza kwa kuzoa mili. 20/- za goli la Mama

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dar

USHINDI wa mabao 4-0 ambao Yanga imepata dhidi ya Vital’o ya Burudi umeifanya timu hiyo kuwa ya kwanza kuzoa kitita cha sh. milioni 20 za goli la Mama.

Mchezo huo ulichezwa juzi kwenye Uwanja Azam Complex,, Chamazi, jijini Dar es Salaam, ambapo kwa ushindi huo Yanga licha ya kujiweka kwenye nafazi nzuri ya kufuzu hatua inayofuata, lakini pia imepata sh. milioni sh. za goli za Mama.

Kama ilivyokuwa msimu uliopiya Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kutoa bonasi kwa kila goli katika mechi za kimataifa ambazo matokeo yake ni ushindi kwa timu za Tanzania, ambapo kila goli ni sh. milioni 5.

Yanga ilikabidhiwa kitita hicho cha sh. milioni 20 na Katibu Mkuu Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni, Gerson Msigwa, ambazo alikabidhiwa Rais wa Yanga, Hers Said, kama zawadi ya ushindi kutoka kwa Rais Samia.

Alisema fedha hizo ni utaratibu Rais Samia kwa vilabu vya Tanzania vitakavyoshinda katika mechi zao za Kimataifa.

Kwa ushindi huo Yanga imejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu raundi ya kwanza katika michuano ya Ligi Mabingwa barani Afrika.

Kimahesabu Yanga inahitaji sare katika mchezo wa marudiano utakaochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa wiki ijayo. Yanga na Azam zinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Simba na Coastal Union zikicheza Kombe la Shirikisho.