Na Yusuph Mussa,Timesmajiraonline,Handeni
SHIRIKA la World vision Tanzania limeweza kuwasaidia wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu kuongeza uwezo wao wa Kusoma na Kuandika (KK) kwenye shule za msingi 11 zilizopo Tarafa ya Mkumburu, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Ambapo uwezo wa kujua kusoma na kuandika kwa watoto hao kupitia Program ya Makambi ya Usomaji katika jamii na kupitia mradi wa kufungulia usomaji yaani Unlocking Literacy, umepanda kutoka asilimia 42 mwaka 2023 hadi kufikia asilimia 62, Machi, mwaka huu 2025.

Hayo yalisemwa Septemba 4, 2025 na
Msimamizi wa Mradi wa Elimu, Mkumburu AP, Shirika la World Vision, Kanda ya Kaskazini, Steward Mwilenga kwenye Kongamano la Program ya Kufungulia Usomaji kwa mwaka 2025 lililofanyika Kijiji cha Ugweno, Kata ya Kwedizinga.
“Kupitia mradi wa kufungulia usomaji yaani Unlocking Literacy wenye lengo la kuimarisha ufunzaji wa kusoma na kuandika kwa sasa unatekelezwa katika vijiji vinane (8) yaani Masatu, Ugweno,Kwedizinga, Taula, Bondo, Kwamgwe, Kwadoya na Ngojoro, pia kwa mwaka wa fedha wa 2025, mradi ulikuwa unatekelezwa katika shule 11 ambazo ni Masatu, Ugweno, Kwedizinga, Taula,
Kwalaguru, Bondo, Kwamgwe, Muungano, Kigoda, Juhudi na Ngojoro, juu ya usimamizi wa makambi pamoja na shule hizo unaendelea.

“Pia program ya kufungulia usomaji ilianza kutekelezwa mwaka 2018 katika Mradi wa Mkumburu. Mradi una jumla ya makambi 17 ambayo ni Mgongola A na B, Kwabojo, Majanini, Kwachifu,
Mkuyuni, Nkumbi, Kwediwandu, Tabora, Msangeni, Kwaboy, Msikitini, Kwedihahi, Mbuyuni, Mnyundo, Simbani na Kwalaguru” amesema Mwilenga
Mwilenga amesema kongamano la program hiyo ya elimu ambalo linawashirikisha wanafunzi, wazazi, viongozi wa vijiji, maofisa elimu kata, hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuongeza umahiri katika ujifunzaji wa Kusoma na Kuandika kwa watoto wa darasa la kwanza, la pili na la tatu,
pamoja na kuwatia moyo walimu wa kujitotelea (Reading Camp Volunteers), wazazi na walimu,wa darasa la kwanza, pili na tatu, pamoja na viongozi wa jamii ili kuwa na ubora wa huduma za elimu kwa maendeleo endelevu.
Mwilenga amesema katika utekelezaji wa shughuli za program ya kufungulia usomaji, baadhi ya shughuli zinazotekelezwa kupitia mradi huo wa kufungulia usomaji ni kufanya tathmini ya usomaji kwa shule zinazolengwa katika A, kutoa mafunzo kwa waratibu elimu, walimu wakuu na wathibiti ubora juu ya ushauri na ufundishaji, kusaidia ufuatiliaji na ufundishaji kwa walimu wakati wa ukusanyaji takwimu kwa kutumia mfumo wa kimataifa wa MEQA

“Kuwezesha mafunzo ya uundaji wa zana za kufundishia kwa walimu wa K.K, ambapo jumla ya walimu 21 walipewa mafunzo hayo Kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa makambi juu ya mbinu za ufundishaji mradi wa K.K
(wasimamizi 20), ununuzi wa vifaa vya kazi kwa walimu wa makambi Gunboot, Mwamvuli, Koti (sh. 4,200,000) Kufundisha walimu wa makambi juu ya uundaji wa zana za kufundishia (Walimu 53, wanaume 18, na wanawake 35).
“Kuwezesha kufanyika kwa warsha za wazazi juu ya msaada wa wazazi kwa watoto kuhusu maendeleo ya ujifunzaji katika Programu ya Kufungulia Usomaji (UL) (375 – wanaume 85, wanawake-290). Ununuzi wa vitendea kazi katika makambi na usambazaji kwa makambi yanayoanzishwa au kuendelezwa
(sh. 4,407870). Kuwezesha kamati za CVA kufanya uhamasishaji kwa wazazi juu ya uandikishaji, sera ya elimu na
malezi bora (415 wazazi –wanawake 248, wanaume 167)” amesema Mwilenga.
Mafanikio yaliyopatikana kupitia utekelezaji wa mradi, ni kujengea uwezo walimu wanaofundisha darasa la kwanza hadi la tatu juu ya mbinu mbali mbali za ufundishaji (Unlock Literacy boost teaching skills), mfano jumla ya walimu 28, ambapo wanaume 11 na wanawake 17 wamejengewa uwezo huo na wanaendelea kuutumia madarasani.
Idadi ya walimu wa kujitolea katika makambi inazidi kuongezeka, pamoja na kuwa wanajitolea hii ni kutokana na mafunzo mbali mbali ambayo yamekuwa yakitolewa hasa juu ya umhimu wa kusaidia jamii kwa njia ya kujitolea, jumla ya walimu hao ni 60, wanaume wakiwa 20 na wanawake 40

“Motisha kwa walimu wa kujitolea juu ya ununuzi wa vifaa vya kazi kwa walimu wa makambi Gunboot, Mwamvuli, Koti (sh. 4,200,000), kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaojua kusoma na kuandika kwa ufasaha kutoka asilimia 42 mwaka 2023 mpaka 62 mwaka 2025, kupitia mradi mdogo yaani PNs. Mradi umefanikiwa kupata mradi wa ujenzi wa
matenki ya kuvunia maji (Water Harvest Tank) katika shule saba za msingi ambazo ni Kigoda, Muungano, Mzule, Juhudi, Masatu, Ugweno, Taula pamoja na ujenzi wa vinawia mikono yaani Hand washing facility katika shule za Kwalaguru, Kwedizinga,
na Mzule, mradi umegharimu sh. milioni 245.
“Kuwajengea uwezo wanajamii/walimu wa kujitolea juu ya mbinu mbali mbali za
usimamizi wa makambi na ufundishaji mfano jumla ya walimu 53 (wanaume 18 na wanawake – 35) wamejengewa uwezo huo, kuongezeka kwa ushiriki wa jamii katika kusimamia miradi ya maendeleo zikiwemo kambi za usomaji, mfano jumla ya wazazi 375 (167 wanaume, 248 wanawake wamekuwa
wakishiriki shughuli hizi, kuimarika kwa matumizi ya zana za kufundishia (Utajiri wa zana) na madarasa
yanayoongea kuanzia kwenye shule husika, makambi. Karibia shule zote na
Makambi zina utajiri wa zana” amesema Mwilenga.

Amesema pia ni kusaidia ujenzi wa vyoo katika shule zenye uhitaji mfano katika shule ya Masatu, mradi
umesaidia ujenzi wa vyoo kwa wavulana na wasichana vyenye matundu manane (8) na thamani yake ni sh. milioni 84.
Kusaidia vifaa mbali mbali katika shule na makambi kama vile vifaa vya michezo, ambapo kila kambi imekabidhiwa mipira miwili pamoja na shule zilizopo ndani ya
mradi ili kuimarisha michezo shuleni.
Mwilenga amesema moja ya changamoto ni mwitikio mdogo wa wazazi juu ya kusaidia shughuli za kielimu katika jamii hali inayofanya watoto wengi kutozingatia masomo yao kwa weledi, mahudhurio hafifu ya watoto katika makambi, bajeti ndogo ya mradi katika kuboresha miundombinu ya shule, miundombinu haba ya madarasa, madawati pamoja na vitendea kazi vingine, idadi ndogo ya walimu kwa baadhi ya shule, ukosefu wa shule shikizi kwa baadhi ya maeneo ambayo shule mama zipo mbali
mfano. Kitongoji cha Kwachifu Kijiji cha Bondo ambacho kipo mbali na shule mama.

“Shirika la World Vision litaendelea kuwa bega kwa bega katika kuunga jitihada za serikali kwa kufanya kazi kwa vitendo, pamoja na kushirikiana na wadau wengine kwa lengo la kusaidia
kuimarisha huduma za jamii kupitia miradi mbali mbali inayotekelezwa katika jamii zetu” amesema Mwilenga.
Naye Afisa Elimu, Shirika la World vision Tanzania, Akaunsia Munuo amesema mradi huo umepata mafanikio na muitikio mkubwa sababu jamii ya Tarafa ya Mkumburu kuanzia wazazi, wanafunzi, viongozi wa vijiji na kata bila kusahau ngazi ya halmashauri, wameupokea kwa mikono miwili, hivyo ametoa wito mradi huo uwe endelevu hata kama siku moja Shirika la World Vision litakuwa halipo, kwani mradi huo ni msaada mkubwa kwa watoto kuweza kujua kusoma na kuandika wakiwa bado wadogo.
Mgeni rasmi, Afisa Uthibiti Ubora Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Morris Maro aliwataka wazazi na wanafunzi kuweza kutunza vifaa vilivyotolewq kwa ajili ya kuwasaidia watoto waweze kusoma, kwani Taifa la Tanzania linamjali mtoto kwa ajili ya kupata stahiki zote ikiwemo elimu, hivyo wazazi waendelea kutoa ushirikiano kwa shirika hilo ili kufanikisha azma ya kuhakikisha watoto wote wanafikia asilimia 100 kujua kusoma na kuandika pindi wakifika darasa la tatu.
Kwenye kongamano hilo, watoto 33 waliofanya vizuri kuanzia la kwanza hadi la tatu kwenye shule 11 walipewa zawadi ya mabegi. Pia walimu 60 wakujitolea walipata vyeti, mabegi na shuka, na walimu 30 wanaofundisha darasa la kwanza hadi la tatu kwenye shule hizo 11 pia walipewa zawadi hizo ikiwemo wazazi sita waliofanya vizuri.


More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi