January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wolper: Wivu ndio kila kitu kwenye mapenzi

MSANII wa filamu na Mjasiriamali hapa nchini Jacqueline Wolper amesema, hakuna kitu kizuri kama wivu kwenye uhusiano wa kimapenzi, kwani ndiyo unaoleta hamasa.

Amesema, ukimuona mtu kwenye mapenzi hamuonei wivu mwenzake ujue mapenzi hakuna, ndio maana yeye ameona wivu ni muhimu sana kwake.

“Wivu kwangu ni muhimu sana, bila ya hivyo naona kama hakuna mapenzi vile, maana raha uulizwe uko wapi, uko na nani, nitaku peleka hakuna kwenda mwenyewe, hayo ndiyo mambo ya kwenye mapenzi,” amesema Wolper.