Na Bakari Lulela,Timesmajira
WAKALA wa vipimo mkoa wa kinondoni jijini Dar es salaam wamekamata wafanyabiashara 2 waliokutwa na kosa la kuuza bidhaa ya nyama kwa kutumia mizani yenye kupunja uhalali wa vipimo.
Akibainisha hayo jijini meneja wa Wakala wa vipimo mkoa wa kinondoni Bi Lilian amesema Leo machi 1,2025 wamefanya zoezi la kawaida la ukaguzi wa kustukiza kulingana na Sheria ya vipimo sura namba 340 pamoja na mapitio yake ya. Mwaka 2002 na kubaini changamoto za baadhi ya watu ambao si waadilifu kutumia mizani isiyo kuwa na sifa kutoa huduma kwa wananchi.
“Tukiwa katika zoezi letu la ukaguzi wa mabucha ya nyama maeneo ya mbezi Louis kwa msuguli Dar es salaam sisi tulinunua nyama kilo 1 katika bucha la kwanza ambapo tulipata gramu 700 ambapo ilikuwa na mapungufu ya gramu 300,”, amesema Lilian
Aidha meneja huyo ameeleza kuwa waliponunua bidhaa hiyo kwenye bucha la pili kwa kiasi cha kilo 2 ikaleta gramu 1600 badala ya gramu 2000 ambapo ilionekana imepunjjwa kwa gramu 400 hii imeonekana kwamba mizani mingi huwa haizingatii uhalali wa vipimo kwa wateja ambao ndio watumiaji wa bidhaa hiyo.

Hata hivyo kulingana na utaratibu wa Sheria za Wakala wa vipimo hufanya ukaguzi mara moja kwa mwaka na kaguzi wa kustukiza mara kwa mara hivyo wafanyabiashara hao wameshikiliwa kutokana ubadhilifu wa kutumia vipimo visivyo halali kwenye bidhaa halisia.
Alidai kuwa mara nyingi watu hao wanapowakamata hufuata utaratibu wa uhakiki wa bidhaa yenyewe na kipimo husika kwa kubaini ujazo na uzito vinaendana ama haviendani.
Hivyo watu hao ambao hukiuka Sheria za vipimo kwa makusudi kabisa hivyo huwashitaki kwa kuwalipisha faini au hupelekwa mahakamani kutokana na tatizo husika.
More Stories
UVCCM waonywa kuwa ‘machawa’
Wahifadhi Wanawake wa TAWA Watembelea Pori la Akiba Wami-mbiki
Halmashauri Rungwe yapongezwa nafasi ya kwanza matokeo kidato cha nne