January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wizara ya ujenzi yatakiwa kupokea barabara zilizopimwa

Na Zena Mohamed,Timesmajira Online,Dodoma

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson, ameitaka Wizara ya ujenzi kupokea barabara za lami kutoka kwa Wakandarasi zikiwa tayari zimeshapimwa ubora wake kwa kiwango kinachofaa kwa matumizi.

Dkt.Tulia amesema hayo jiji hapa leo Mei 27,2024 wakati alipotembelea na kuzindua maonesho ya taasisi mbalimbali za sekta ya ujenzi zilizopo chini ya Wizara ya Ujenzi ambapo amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kwa ajili ya vifaa vya kisasa vya kupimia barabara hivyo hawatarajii kuona barabara inakabidhiwa bila kupimwa.

“Nilipotembelea hapa niliuliza hivi vifaa vya kisasa vilinunuliwa lini nimeambiwa vilinunuliwa mwaka mmoja uliopita au miaka miwili iliyopita ni vifaa hivyo vimenunuliwa kipindi cha serikali hii ni vifaa ambavyo vinatuondoa kwenye changamoto ambayo barabara ingeweza kupokelewa na Wizara bila kupimwa,”.

“Mkandarasi ameshamaliza anakabidhi halafu mvua inanyesha kipindi kimoja barabara imeshaweka mashimo kwaio sisi wabunge tunalazimika tena kuanza kutafakari namna ya kuishauri serikali ama kuisimamia serikali kwamba mlipokeaje barabara kama hii lakini kumbe vifaa tulikuwa hatuna vya kupima nakuoana kwamba ubora wa hii barabara tangu inapoanza kujengwa na matabaka yote yanawekwa na je yamewekwa kwa vipimo vinavyotakiwa na sasa kwakuwa tunavyo vifaa hivi nimeona magari hapo nje yaashiria barabara hazitapokelewa kabla ya vipimo,”amesema Dkt.Tulia.

Amesema kuwa kwakuwa magari yamenunuliwa zile changamoto zilizokuwa zinaonekana mwanzo hazitaonekana tena kwamba barabara mpya lakini mashimo yanaanza kuonekana na mvua imenyesha tu mara moja halafu serikali pesa imeshatoa tunaanza tena kupitisha au kusikiliza tena bajeti ambayo inaonesha hiyo barabara itengewe fedha upya.

“Sasa leo mambo yaliyozungumzwa hapa ni yakitaalamu sana hivyo mkayafanyie kazi,”Naweza kutolea mfano barabara hii ya Iringa-Dodoma huwa napita sana hiyo barabara kunakipindi tukajua hiyo barabara imekamilika mashimo yakaanza ,mashimo yale yakaenda mpaka ile barabara ilibidi ijengwe upya na hii barabara haina umri huo ambao ingestahili kuanza kujengwa upya sasa nina aamini vifaa hivi ambavyo mmetoa salamu kwa mheshimiwa Rais za kumpongeza na mimi kwasababu nimekuja hapa kutembelea basi nimezipokea,”amesema.

Aidha amesistiza kuwa ni muhimu hivyo vifaa vikafanye kazi iliyokusudiwa na wao hawatarajii kwani nchi kwa upande wa Tanzania Bara inamajimbo 214 na kwahivyo hakuna mahali barabara itapita Mbunge asijue kwamba barabara imekamilika.

“Hatutarajii kuanzia sasa baada ya hivi vifaa kuanza kujikuta mazingira ambayo umepokea barabara kabla hamjapima halafu mnakuja tena kuomba fedha kwajili ya marekebisho ya hizo barabara,”.

Pamoja na hayo amewataka Mameneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) wa mikoa yote kutoa taarifa kwa haraka kwa barabara ambazo zinahitaji matengenezo ya dharura ili tusilazike kutengeneza barabara upya kwenye yale maeneo ambayo yangeweza kutengeneza mashimo na hali ingekuwa mazuri.

Pia alimpongeza Rais kwa kazi nzuri anayoifanya kwenye uwekezaji kwenye eneo hilo la miundombinu ya barabara.

“Sote tunafahamu miaka miwili iliyopita Rais alipewa tuzo maalumu ya miundombinu kwenye eneo la barabara na sasa tuzo ile bila shaka kwa maonesho haya imeonesha namna ambavyo tumepiga hatua,”.