Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Imeelezwa kuwa waandishi wa habari wananafasi ya kufahamisha jamii juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi,hivyo wito umetolewa kutumia kalamu zao kuelimisha kuhusu utunzaji wa mazingira nchi kavu na majini.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Uwazi wa Takwimu ambayo yamefanyika jijini Mwanza kupitia chama hicho na ufadhili wa shirika la Open Knowledge Foundation yakiwa na kaulimbiu isemayo ‘Uwazi wa Takwimu kwenye kuimarisha maisha.
Soko amesema,wanaamini waandishi wa habari wakitumia kalamu zao vizuri kuandika juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi yanayopelekea fukwe kuwa na athari kubwa habari itasomwa na kusikilizwa na watu wengi ambao watapata elimu kwa kiasi kikubwa.
Hivyo kwasababu hiyo wakaona ni muhimu kuwalete waandishi wa habari kupitia maadhimisho hayo ili wawaelimishe juu ya umuhimu wa kutumia data katika uhifadhi wa fukwe.
“Fukwe ni biashara inayofanyika sana duniani kote,tumieni kalamu zenu kuhakikisha ajenda hiyo tunaibeba vizuri,tunaelimisha jamii suala la kutunza mazingira kwenye pande zote mbili ya majini na nchi kavu,mkifanya hivyo basi tunaamini uvumilivu katika fukwe zetu utaendelea kuwa mkubwa kupitia elimu tutakayo itoa na serikali itaendelea kutengeneza sera nzuri na sheria nzuri kwa kuhakikisha kwamba suala la mabadiliko ya tabia ya nchi tunalidhibiti hasa kwenye uhifadhi wa fukwe zetu zinaendelea kuwa salama na jamii inaendelea kuzitumia salama,”ameeleza Soko.
Kwa mujibu wa Soko ameeleza kuwa takribani asilimia 57 ya uchumi wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, unategemea shughuli za maziwa na bahari hivyo jamii kutowajibika kwenye utunzaji wa mazingira inaweza kusababisha joto kali ambalo litasababisha fukwe kufunikwa na maji hivyo kurudisha nyuma biashara zinazofanyika katika fukwe.
Kwa upande wake Mratibu OJADACT, Lucyphine Kilanga,ameeleza kuwa ipo changamoto ya matumizi ya takwimu kwenye Habari zinazohusu uhimilivu wa fukwe za bahari na maziwa.
Kilanga amesema,wamepata ufadhili kutoka shirika hilo kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika upatikanaji wa taarifa upande wa fukwe kwani kumekuwa na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo kwa upande wa Kanda ya Ziwa wamekuwa waliona kina cha maji kikiongezeka.
Naye Mmoja wa washiriki wa maadhimisho hayo Mariam John ameeleza kuwa ili kuweza kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi katika fukwe ojadact waandae mkutano ambao utawakutanisha na jamii inayoishi kando kando mwa ziwa ili kuwapatia elimu na kufahamu sababu zinazopelekea wao kutotunza mazingira ndani ya majini
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu