October 9, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wiki ya vijana yageuka kitovu Cha fursa na ubunifu:Rukwa


‎
‎Wajasiriamali kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Rukwa wamepongeza mwitikio wa wananchi na vijana katika maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayoendelea katika viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Sumbawanga Manispaa.
‎
‎Maonyesho hayo yameanza rasmi jana Oktoba 8, na yataendelea hadi Oktoba 18, yakilenga kuwaunganisha vijana, wananchi na wadau mbalimbali kwa ajili ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kutambua fursa zilizopo.
‎
‎Katika maonyesho hayo, wananchi wanaweza kupata huduma mbalimbali, kujionea bidhaa na ubunifu wa vijana, pamoja na kupata maarifa kuhusu fursa za biashara na ujasiriamali.
‎
‎Wajasiriamali wameendelea kutoa wito kwa wananchi na vijana ambao bado hawajafika Ndua kutumia fursa hiyo kutembelea maonyesho na kujifunza mambo mapya yanayoweza kuwasaidia katika shughuli zao.
‎
‎Usibaki nyumbani! Njoo Ndua, tembelea maonyesho ya Wiki ya Vijana hadi Oktoba 18 na ujifunze kitu kipya.
‎
‎