Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala
MKUU wa Wilaya ya Ilala,mkoani Dar-es-Salaam Edward Mpogolo,amewataka Wenyeviti wa Serikali za mitaa wa Wilaya ya Ilala kwenda kutenda haki,kufuata misingi bora na kanuni katika kuwatumikia wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema hayo wakati wa kuwapishwa Wenyeviti wapya wa wilaya hiyo 159 waliopita kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).
“Mmechaguliwa na wananchi, hivyo nendeni mkawatumikie kwa kutoa huduma bora na sio kuwauzia huduma.Wananchi wana imani na ninyi na ndio maana wamewachagua,hivyo mkatende haki kwani kiongozi anayetenda haki eneo lake linakuwa na amani na utulivu,”.
Pia amesema Halmashauri ya Jiji ni miongoni mwa Halmashauri zenye mitaa mingi,uchaguzi ulimalizika kwa amani pasipo vurugu wala vinyongo.
Kwa upande wake Mstahiki Meya Omary Kumbilamoto, amewataka viongozi hao kwenda kusimamia miradi iliyopo katika mitaa yao kwa maendeleo ya mitaa yao na taifa kwa ujumla.
Kumbilamoto,amesema Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za Mitaa wamekula kiapo cha uaminifu, utii ,
katika kutimiza majukumu yao na kuwatendea haki watu wote kwa mujibu wa sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waende wakachape kazi katika kujenga Taifa.
More Stories
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi