Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dar
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga,amefanya ziara ya kutembelea ofisi ya Tume ya Ushindani(FCC), kwa lengo la kuogeza ufanisi katika ufanyaji wa majukumu mbalimbali ya kazi.
Kapinga amefanya ziara hiyo Novemba 24,2025 wakati alipotembelea ofisi za FCC,zilizopo jijini Dar-es-Salaam,ambapo amesema,Tume hiyo inafanya kazi ya kudhibiti, kulinda walaji, bidhaa feki pamoja na utoajia elimu ya masuala ya kibiashara ikiwemo muunganiko wa kampuni kubwa.

Pia kuhakikisha muunganiko huo wa ushindani unaleta manufaa kwenye shughuli za kibiashara.
“Kikao cha leo kinalenga namna nzuri ya utendaji kazi ili kufikia mategemeo na matarajio ya Watanzania ambao ni walaji pamoja na kuongeza njia ya kuwafikia zaidi ili kupata mrejesho wa kazi tunazozifanya kwa urahisi ” amesema Kapinga.
Hata hivyo Kapinga amesisitiza kuwa Tume ya Ushindani wa Udhibiti wa Bidhaa pamoja kudhibiti bidhaa feki wameweka mikakati ya kuongeza ufanisi na ubunifu ili kuboresha utendaji kazi wa FCC.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa FCC,Hadija Kasongwa,amesema tume hiyo inaratibu zaidi ili kwenda na falsafa ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuwezesha vyombo hivyo kutatua matatizo ya wananchi katika ufanyaji wa biashara
Kasongwa amesema katika miaka minne kulikuwa na falsafa ya ukuzaji uwekezaji nchini ambapo taasisi hiyo inapitia na kuchambua miamala ya miunganiko ya kampuni kwa lengo la kukuza mitaji pamoja na kuokoa ajira kwa baadhi ya kampuni na viwanda.
Sanjari na hayo amesema kuanzia Desemba 1,2025 kutakuwa na zoezi la kurekodi usafirishaji wa bidhaa zote zinazoingia nchini hivyo itasaidia kuzichunguza na kudhibiti uingizwaji wa bidhaa feki na zisizokidhi viwango.


More Stories
Kihongosi amtaka mkandarasi kuwalipa vibarua stahiki zao
DC Mbozi afuturisha wananchi, asisitiza mshikamano na Umoja.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Nina imani mubna utendaji kazi wa ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria