Na Mwandishi Maalum, TimesMajira Online.
MADIWANI wa Mji Mkuu wa Ujerumani, Berlin wameridhia kwa kupiga kura kubadilisha jina la barabara iliyokuwa inampa heshima aliyekuwa Gavana wa Afrika Mashariki (kipindi cha ukoloni) na badala yake kuweka jina la mwanaharakati mwanamke mpigania uhuru nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Utangazaji nchini Uingereza, barabara inayojulikana kama Wissman straße, ambalo ni jina la Hermann von Wissmann, sasa itaitwa Lucy-Lameck-Straße.
Lucy Lameck aliwahi kuwa Waziri wa kwanza mwanamke nchini Tanzania ambaye pia alikuwa miongoni mwa viongozi walilopigania uhuru wa Tanganyika.
Wissman alikuwa Gavana wa Taifa la Ujerumani katika Afrika Mashariki ambayo kwa sasa ni mataifa ya Tanzania, Burundi na Rwanda mwisho wa karne ya 19. Kwa mujibu wa gazeti la Der Tagesspiegel la nchini Ujerumani, Wiassman ndiye anadaiwa aliyesababisha mauaji ya wakazi wengi zaidi katika koloni hilo.
Wanaharakati nchini Ujerumani wameunga mkono tukio hilo kwa kutoa taarifa ikisema kuwa kampeni hiyo itaondoa heshima ya ”Von Wissmann na badala yake kupewa heshma mwanamke Mtanzania ambaye alipinga ukoloni na ubaguzi wa rangi”.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Samia avuna makubwa Mikutano ya Uwili G20