Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Afa,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima Amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo na Ushirikiano wa Nchi ya Switzerland Patricia Danzi aliyeambatana na ujumbe kutoka uswisi ambaye ameihakikishia Tanzania kuendelea kudumisha ushirikiano ulioanzishwa tangu mwaka 1920 baina ya nchi mbili.
Katika kikao hicho kwa pamoja wamekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano katika kuketa Maendeleo nchini hususan katika eneo la huduma za afya kwa Watanzania.
Dkt. Gwajima amesema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya inaendelea kuboresha huduma za afya, na sasa ipo mbioni kupitisha sheria ya Bima ya Afya kwa wote itayomruhusu kila mwananchi kuwa na Bima ili kupata huduma za matibabu.
Amesema kuwa Uswisi inatekeleza mradi mkubwa wa Mfuko wa Bima ya Afya ulioboreshwa CHIF kwa maendeleo ya jamii unaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 24.3 utakao tekelezwa katika kilindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2019 hadi mwaka 2023 ambapo Fedha hizo zinatumoka kujenga uwezo kwa watumishi kuelimisha na kuhamasisha jamii
Aliendelea kusema kuwa, kama nchi inaendelea kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria kwa kupitia afua mbalimbali ikiwemo utoaji elimu kwa wananchi juu ya njia bora za kujikinga dhidi ya Malaria na ujenzi wa kuwanda cha viuadudu kilichopo Mkoa wa Pwani ambapo serikali ya uswisi imetowa msaada wa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 15.4 kutekeleza mradi wa kipambana na Malaria mkuwa ikiwemo utoaji wa neti na utafiti
Dkt Gwajima Amesema Nchi ya Uswisi imeendelea kusaidia Tanzania Katika masuala ya Utafiti wa Magonjwa ambapo bajeti ya mwaka 2019 hadi 2024 zimetengwa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 4.8 ambapo Tanzania imeendelea kubiresha huduma kwa kujenga vituo vya afya Zahanati na Hospitali za Rufaa kwa lengo la kudlsogeza huduma kwa jamii.
Amesisitiza kuwa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan amedhamilia kuwakomboa wanawake kiuchumi kwa usawa wa kijinsia ambapo serikali imeandaa mpango kazi wa kuendeleza wanawake ili kuunda juhudi za serikali ya awamu ya sita.
Aidha, Dkt. Gwajima amesema kuwa, Tanzania inaendelea na mapambano dhidi ya UVIKO-19 kupitia afua ya Elimu kwa wananchi juu ya njia bora za kujikinga na maradhi na utoaji wa Chanjo ya UVIKO-19, huku akieleza tayari Tanzania imepokea Chanjo tofauti ikiwemo Jenseen, Sinopharm na Pfizer.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo na Ushirikiano ya Uswisi Patricia Danzi amesema Serikali ya Uswisi imekuwa mdau mzuri wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 kwa kuchangia zaidi ya Dozi 4,000,000 kupitia Shirikisho la Kimataifa la Taasisi zinazoratibu upatikanaji na usambazaji wa chanjo ya uviko 19 ( COVAX Facility ) likijusisha nchi mbalimbali Dunia.
Viongozi hao wamekutana leo, katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma na kikao hicho kimehudhuriwa na baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Afya na Shirikishi la Maendeleo na Ushirikiano Uswisi.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria