December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Ummy aongeza siku 15 za ujenzi wa vyumba vya madarasa

Na Mwandishi wetu,timesmajira,online

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Ummy Mwalimu ameongeza siku 15 kwa Halmashauri zote nchini kukamilisha ujenzi wa
vyumba vya madarasa.

Amesema kwa sasa vyumba vyote vya madarasa katika halmashauri zote nchini vitakabidhiwa Disemba 31,2021 badala ya Disemba 15,2021 kama ilivyoelekezwa hapo awali.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Waziri Ummy imesema baada ya kikao cha tathmini na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Prof.Riziki
Shemdoe na kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi Waziri Ummy ameeleza kuwa mpaka sasa kazi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa inakwenda vizuri na takribani
asilimia 60 wamekamilisha ujenzi na wengine wako katika hatua za ukamilishaji.

“Hata hivyo katika baadhi ya maeneo walikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa vifaa vya
ujenzi hivyo kupelekea kazi ya ujenzi kutokwenda kama inavyotakiwa kwa mujibu wa
muda uliotolewa,kutokana na hali hiyo ameona ni vyema kuongeza muda ili kuzipa fursa Halmashauri
ambazo hazijakamilisha kazi kutumia muda wa nyongeza kukamisha ujenzi wa vyumba
vya madarasa,” amesema