November 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Ummy ahudhuria kikao nchini Ufaransa

Na Mwandishi wetu, Paris, Ufaransa

Waziri wa Afya Ummy,leo tarehe 6 Juni, 2022 amewasili katika Jiji la Paris , Ufaransa kuhudhuria kikao cha Jumuia ya Wafadhili wa Huduma za Afya ya Mama na Mtoto (Global Financing Facility – GFF).

Akiwa nchini Ufaransa Waziri Ummy amekutana na Mawaziri wenzake kutoka Sierra Leone, Bukinafaso, Niger na nchini nyingine kwenye kikao cha kuzungumzia changamoto zinazokwamisha katika utoaji huduma bora.

Akizungumza kwenye kikao hicho Waziri Ummy amesema upungufu wa watoa huduma wenye ujuzi ni changamoto kubwa inayoikabili Tanzania katika kuhakikisha inatoa huduma bora.

Aidha, ubora wa mafunzo yanayotolewa na kile wanachokipata wahitimu ametaja kuwa ni tatizo linalochangia kwenye matokeo yasiyotarajiwa kwenye vituo vya kutolea huduma.

Ameongeza kuwa Tanzania ina shida kwenye kutumia watoa huduma ngazi ya jamii wakati uzalishaji wa watoa huduma wenye ujuzi likiwa kubwa. Swali linagonga vichwa ni je “tumchukue asie na ujuzi au mwenye ujuzi” ili kuweza kupata matokeo yenye tija zaidi