Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wameanza kutekeleza Mradi wa kuendeleza uvuvi na ufugaji samaki (TASFAM) wenye thamani ya Tsh. Bilioni 312.
Waziri Ulega amesema hayo leo Agosti 20, 2024 wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya uvuvi na tasnia nyingine kuelekea Tamasha la Kizimkazi linaloendelea, Kizimkazi, Zanzibar.
“Baadhi ya kazi zitakazotekelezwa na mradi huu ni pamoja na Kutoa ufadhili wa Masomo kwa Watoto wa Wavuvi kwa kuwasomesha katika ngazi za ufundi, Cheti, Diploma na Shahada ili waweze kujiajiri katika sekta nyingine na kupunguza utegemezi katika bahari pekeyake”, amesema
Pia, Kuendeleza maudhui ya BBT kwa kutoa mafunzo ya ufugaji majongoo bahari, unenepeshaji wa kaa, ufugaji wa chaza wa lulu na kilimo cha mwani, Kununua na kugawa boti na vifaa vya uvuvi, boti 270 na zana za uvuvi kwa vikundi vya wavuvi na wakulima wa mwani”, ameongeza
Halikadhalika, Waziri Ulega alibainisha kuwa, sera na mikakati ya uvuvi iliopo nchini inalenga kuimarisha usimamizi wa rasilimali za uvuvi na mazingira ya bahari huku akitoa shime kwa jamii kuhakikisha kwamba rasilimali za baharini zinatunzwa na kulindwa vizuri kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo kwa kufanya matumizi endelevu ya rasilimali hizo na kupambana na uvuvi haramu.
More Stories
Mtendaji afukuzwa kazi kwa rushwa
Mwalimu aliyetuhumiwa kumbaka mwanafunzi wake atiwa mbaroni
Vyuo Vikuu Dar vyatambulisha tamasha la UNIFEST 255