November 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Ndejembi awafunda watumishi wa serikali waliohitimu mafunzo ya uongozi

Na David John, TimesMajira Online

SERIKALI imewataka wahitimu wa Mafunzo ya Stashahada Uzamili ya uongozi pamoja na Mafunzo ya uongozi kwa Njia ya mtandao kwa ngazi ya cheti kwenda kutumia vizuri elimu waliyoipata na kwenda kuonyesha kwa vitendo kile walichojifunza.

Imesema kuwa mafunzo ya maisha mategemeo yao ni makubwa kwa wahitimu hao na sasa wanataka kuona uongozi wa kimkakati, kusimamia vizuri rasilimali watu na fedha,lazima wakafanye mabolesho katika nyanja ya mawasiliano na mahusiano

Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar Es Salaam na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Deogratius Ndejembi katika mahafali ya tano ya Mafunzo ya Stashahada ya Uzamili ya Uongozi na mafunzo ya uongozi kwa njia ya mtandao kwa ngazi ya cheti yanayotolewa chini ya Tasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na chuo cha Aalto EE cha Nchini Finland.

Waziri amesema kuwa ” Nchi yetu ina rasilimali mbalimbali, yakiwemo Madini, Mito, Bahari, mimea na rasilimali hizi ziwe na manufaa kwa taifa lazima kuwe na watu wenye weredi wa kutosha hivyo mafunzo haya ni sehemu ya kuwajengea uwezo kwaajili ya kusimamia raailimali zetu kikamilifu”amesema

Nakuongeza Kuwa “kiongozi mzuri ni yule anayewajibika na kutekeleza,kujituma na majukumu yake bila kushurutishwa.

Ameongeza Kuwa mategemeo ni kuona utumishi bora, wenye msingi imara na thabiti kiuongozi, kiutendaji mara baada ya kurejea sehemu zao za kazi.

Pia ametumia siku hiyo Kuwa karibisha washiriki wa awamu ya sita katika mafunzo ya uongozi Kwani Matumaini yake ni kuona washiriki wapya wanafuata nyayo za waliowatangulia na ikiwezekana wafanye vizuri zaidi .

Naibu waziri Ndejebi ameiomba Taasisi ya Uongozi kuandika tawasifu za Marais waliomaliza tawala zao akiwamo Rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete na Rais wa awamu ya tano, Hayati Dkt. John Magufuli,huku akiwapongeza kwa kazi kubwa wanayofanya.

Kwa upande wa Katibu Mkuu Kiongozi Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said ametoa ra kwa. viongozi kutokuwa wabinafsi pale zinapotokea fursa mbalimbali katika jamii.

“Hapa niseme kidogo wengine wanakuwa wanajali wa Kwao na Jamaa zao.. wengine husema kutesa kwa zamu kwakuwa mwezao yupo juu pale Amesema mhandisi Zena

Amesema viongozi wengine wanafikilia kuwa Uongozi ni kama ajira ya kawaida na kupata mshahara wake, kumbe dhima kubwa ya Uongozi ni kuonesha njia kwa wengine mfano mahali popote penye kiongozi panatakiwa kujulikana kama yupo.

Amefafanua kuwa kiongozi anatakiwa kuwa mtu wa kuwatia moyo wengine walio chini yake ili waweze kuendeleza vipaji vyao, sio kuwavunja moyo au kuwa na kauli za kudharau na kukatisha tamaa katika kazi na jitihada wanazojaribu kuonesha mahali pa kazi.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute,) Dkt. Kadari Singo amesema, Taasisi hiyo ina jukumu kubwa la kuandaa na kuendesha mafunzo kwa viongozi, kuendesha majadiliano ya kisera na kufanya tafiti za kisera, kutoa ushauri wa kitalaam na kusaidia taasisi mbalimbali pamoja na viongozi wake katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute,) ilianzishwa Julai, 2010 kwa malengo ya kuwa na kituo cha utalaam wa juu cha kuendeleza viongozi barani Afrika kwa kuanzia nchini Tanzania, Kanda za Afrika Mashariki na Afrika nzima.