Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 17 y Chuo cha Kodi (ITA) ambapo atatunuku vyeti, Stashahada, Shahada na Stashahada ya Uzamili kwa wahitimu 417 wa mwaka wa masomo 2023/2024
Akizungumza na waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Isaya Jairo amesema Mahafali hayo yatafanyika chuoni hapo ambapo mbali na Waziri kutunuku vyeti, pia atatoa zawadi kwa wahitimu na wanafunzi wanaoendelea na masomo waliofanya vizuri zaidi katika mwaka wa masomo 2023/2024 pamoja na wahadhiri wa chuo waliotoa machapisho mbalimbali.
Amesema kuwa wahitimu 195 watatunukiwa cheti cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki, wahatimu 28 watatunukiwa cheti cha usimamizi wa forodha na kodi, wahitimu 61 watatunukiwa stashahada ya usimamizi wa forodha na kodi na wahitimu 119 wakitunukiwa shahada ya usimamizi aa forodha na kodi.
Prof. Jairo amesema Chuo cha Kodi kinajivunia mafanikio mengi katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tano wa Chuo ambao umejikita katika kutoa matunzo kwa njia ya kisasa za kidijitali.
“Tunatarajia mafunzo ya elimu masafa (onlineDistance Electronic Learning) yatakapoanza yataongeza idadi ya wanafunzi wanaopata mafunzo katika chuo pamoja na kufikia wanafunzi wengi kwa njia rahisi, kwa wakati mmoja na kwa gharama nafuu na hivyo kuongeza idadi ya wahitimu” amesema
Jairo amesema kuanzishwa kwa mafunzo hayo kielectroniki ya masafa huria mwaka huu utasaidia kuongeza uandikishaji wa wanafunzi kwa mwaka kutoka 5000 hadi 7000 na kupanua ufikiaji wa programu maalim za mafunzo ya ITA.
Aidha ameibanisha ushirikiano wa ITA na somaliland katika kutengeneza mfumo thabiti sa usimamizi s forodha ma kodi.
Amesema kuwa kufanya kazi na nchi kama Somaliland, Zanzibar,Bostwana na malawi, ITA Inaendelea kuchukua jukumu muhimu katika kuboresha ukusanyaji wa mapato na kuimarisha mifomo ya modi barani Afrika.
More Stories
Waziri Mavunde awakaribisha wawekezaji wa madini kutoka Finland
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar azindua kampeni Katavi
Wahitimu 417 watarajiwa kutunikiwa vyeti ITA