Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga
Waziri Nape amesema serikali ina mpango wa kukigeuza kijiji cha Msomera kuwa kijiji cha kisasa na cha kidigitali.
Akiongea Wakati wa uzinduzi wa mnara wa muda Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Habari Nape Nauye alisema kuwa Serikali itaendelea kusogeza huduma za Mawasiliano ya uhakika katika vijiji na maeneo yasiyopewa kipaumbele kwani bila mawasiliano hakuna maisha.
Alisema kuwa Serikali Kwa kushirikiana na makampuni ya huduma za simu itahakikisha inaendelea kusogeza huduma karibu na wananchi hususani kwenye maeneo yote ambayo yanachangamoto za kimtandao.
“Lengo la serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania popote pale alipo anapata huduma Bora za Mawasiliano bila ya kujali eneo ambalo lipo kwani eneo ambalo linamtandao linamaendeleo makubwa”alisema Waziri hiyo.
Kwa mujibu wa Waziri Nape alisema TTCL imepanga kukamilisha kazi yake ya kujenga mnara wa mawasiliano ifikapo mwisho wa mwezi huu (Julai).
Alisema serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasssn imedhamiria kutimizaahadi yake na kufanikisha mpango huo. ‘Anakifanya kile ambacho wengine walidhani hakiwezekani Kuhamisha watu kutoka Ngorongoro kwa amani na kwa hiari yao nakutoa huduma zote muhimu,” Nape alisema.
Aidha alitoa wito kwa wakazi wa Ngorongoro wanaohamia kwenye makazi yao mapya kuwapuuza wapinzani wanaotaka kupaka matope programu hii.
“Inashangaza mtu ambaye hajavaa kiatu anataka tuamini kuwa anasikiauchungu kwa niaba yetu,”
Nape aliongeza na kusema kuwa watu wa njehawawezi kujifanya wanawapenda watu wa Ngorongoro kuliko serikaliambayo imetafuta mabilioni ili kuhakikisha kuwa wanahama kwa amani,”alisisitiza Waziri Nape Nnauye.
Aliagiza taasisi zote zilizo chini ya wizara yake zifungue huduma kijijini hapo mara moja, ikiwa ni pamoja na TTCL, Shirika la Posta na wengine.
Nape alisisitiza kuwa serikali imedhamiria kukigeuza kijiji hicho kuwamfano na cha kisasa cha vijijini ambacho kitafunguliwa fursa za maendeleo kwa wote.
Hata hivyo Waziri Nape aliiagiza TCRA kuimarisha mawasiliano ili watu wa Msomelawanaweza kufurahia mawasiliano mazuri ya redio na Televisheni.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya Handeni Sirieli Mchembe alisema Msomelaitakuwa kituo kikuu cha biashara na mipango ya kuboresha miundombinuya barabara ikiwa ni pamoja na ukarabati wa barabara inayounganishaeneo hilo na Mombo wilayani Korogwe, katika Barabara kuu ya Tanga -Arusha.
Mnara huo, kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Airtel,Beatrice Singano, ni wa muda unaolenga kuhakikisha wanakijijiwanafurahia manufaa ya mawasiliano ya kisasa.
Mkuu wa kitengo Cha Mawasiliano kutoka kampuni ya simu za mkononi Airtel Beatrice Singano alisema kuwa katika kuunga mkono juhudi za serikali wameamua kusogeza huduma za simu na mtandao kwenye eneo hilo.
Singano alisema kuwa ufungaji wa mnara huo wa muda utafungua fursampya ikiwa ni pamoja na huduma za kuhamisha fedha ambazo hapo awalihazikupatikana kijijini kutokana mawasiliano duni.
Alisema wanasubirikukamilika kwa mnara wa TTCL kuunganisha mawasiliano yao kupitiamnara.
“Tulitaka kuwa sehemu ya mchakato wa maendeleo pale Msomela,” alisemana kuongeza kuwa waliona ni wajibu wao kuwa wa kwanza kupelekamawasiliano ya kidijitali kwa sababu serikali ina hisa asilimia 49katika kampuni hiyo.,”alisisitiza
Mkazi mpya wa Ngorongoro ambaye amefungua kibanda cha huduma yaAirtel, Juliana Luka alisema kuwa walikuwa na furaha hapa kwa sababusasa wako huru kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo za kilimo ambazohawakuweza kufanye Ngorongoro.
Diwani wa Kata ya Kalkesio iliyopo Ngorongoro, Ole Tiamas na madiwaniwengine wawili, Veronica Mafruda (Viti Maalum) na Augustine Rumas waKata ya EYASI nao ni baadhi ya watu ambao wameamua kuonyesha mfanowakuhamakwa hiari.
Walisema walivutiwa na walichokiona kinyume na hadithi ambazo wamekuwawakisikia kutoka kwa wapotoshaji.
“Tuliambiwa kwamba tutugua mara tutunapofika hapa lakini bado tuna afya njema na hakuna aliyeripotiwakuugua,” alisema
OletiamasiMsomela, kijiji ambaco kimeanza kupokea wanakijiji wapya kutokaNgorongoro leo kimeadhimisha mnara wake wa kwanza wa mawasilianokutoka Airtel ambao umeelezwa kuwa utafungua kijiji kupata fursa zamaendeleo.
Mnara huo ambao ni wa muda ulizinduliwa na Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia, Nape Nnauye katika hafla hiyo kijijijinileo.
More Stories
AU yaipatia Tanzania Dola za Kimarekani 200,000 mchango Maafa Hanang
NIC yazindua msimu wa pili kampeni ya NIC KITAA
CCM: TAMISEMI puuzeni makosa madogo madogo ,kukuza Demokrasia