Na David John,TimesMajira Online
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango amelipongeza Shirika la Madini Tanzania STAMICO kwa kuwa wabunifu na kuchukua tuzo ya ushindi wa jumla katika maonyesho ya Kimataifa ya 45 ya Biashara Sabasaba.
Dkt.Mapango ametoa pongezi hizo mara baada ya kufungua maonyesho hayo jana nakwamba Shirika la Madini la Taifa STAMICO limefanikiwa kuchukua tuzo hiyo kwa kuwa wamekuwa wabunifu lakini sio wao tu bali hata taasisi nyingine kama vile wadhamini wakuu wa maonyesho hayo Benki Kuu ya Tanzania BoT,COSTECH pamoja na Benki ya Biashara NBC ambao ni wadhamini wakuu wa maonyesho hayo.
Naye Waziri wa Wizara ya Madini Dotto Biteko akizungumza mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Madini hususani STAMICO amesema kuwa ili kuweza kufanya vizuri katika sekta ya madini ni muhimu kutengeneza mfumo ambao utawezesha kufanyika Kwa biashara ya Madini Kwa umakini.
Waziri Biteko ameongeza kuwa sekta ya madini iko vizuri na salama na matamanio yake ni kuona sekta hiyo inachangia zaidi kwenye pato la taifa.
“Natamani kuona namba zinaongezeka zaidi tumetoka asilimia mbili hadi sasa tuko asilimia tano kwenye pato la taifa na itakapofika miaka mitatu ijayo tutakuwa mbali sana kwani tunamuamini Mungu katika hilo”amesema
Akizungumzia shirika hilo na mikakati mbalimbali ya kuwawezesha wadau kupitia sekta ya madini Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Dkt.Venance Mwasse amesema wanajisikia furaha kuchukua tuzo hiyo na imewapa chachu ya kuendelea kuwa bora nyakati zote kama wadau wanavyofahamu kuwa shirika hilo ndilo linashughulikia masuala ya madini nchini.
Ameongeza kuwa Shirika la Madini la Taifa STAMIC kama yalivyo mashirika mengine wameshiriki katika maonyesho hayo ili kuwaeleza watanzania shughuli mbalimbali zinazofanywa na ukizingatia kwamba shirika hilo ni muhimu sana na hivi sasa wamekuwa wakiwawezesha wachimbaji wadogo hususan viziwi katika kuhakikisha nao wanashiriki katika shughuli za madini.
Pia akizungumzia mradi wa mgodi wa Kiwila wa makaa ya mawe ambao unatarajia kuzalisha mkaa kwa matumizi ya majumbani , wamejipanga vizuri ili kuona mradi huo unawafikia watanzania na unakuwa tiba katika uharibufu wa mazingira wa ukataji wa miti kwa ajili ya kuni.
Amesema lengo na juhudi zinazofanywa na shirika nikuhakikisha wanawashika mkono wachimbaji wadogo na ndio maana wameaza na wachimbaji wadogo viziwi walioko kule mkoani Geita ili kuwafanya nao wanakuwa wachimbaji wakubwa hapo baadae.
More Stories
Wafanyabiashara wakutana Dar,kujadili hali ya biashara
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar
CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo