December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri, Mkuu wa mkoa Mbeya wataka GF Trucks & Equipment’s Ltd Kufungua ofisi Chunya

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Naibu waziri wa Madini, Steveni Kiruswa na mkuu wa mkoa wa Mbeya wameutaka uongozi wa kampuni ya uuzaji wa Magari ya mizigo na Mitambo ya kuchimbia madini GF Trucks kuhakikisha wanafungua ofisi (Yadi) ya kuuzia mitambo jirani na migodi ili kuwafikia wahitaji kwa haraka.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Teknolojia ya madini yaliofanyika mkoani Mbeya katika Wilaya ya Chunya alizitaka kampuni zinazotoa huduma za kuuzaji wa vifaa mbalimbli vya migodini kufungua ofisi jirani ili kuweza kuwarahisishia wanunuzi ambao ni wachimbaji wadogo upatikanaji wa vifaa hivyo kwa wakati.

Akikazia kauli yiyo Mkuu wa mkoa wa Mbeya aliiotaka GF Kuhakikisha wanachangamkia fursa ya kufungua ofisi jirani na machimbao hayo kwani kwa kufanya hivyo itarahisisha wao kukutana ana mteja mara kwa mara na sio kusubiri hadi wakati wa maonyesho.

Nae Afisa Mawasiliasno wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd,Smart Deus aliseme wameipokea kama maagizo kauli hiyo ya viongozi na wanaamini muda sim mrefu watafungua ofisi katika maeneo hayo ili kuwa karibu na wateja wao.

GF inajivunia kuwa wauzaji wa mashine za migodini (greda) aina ya XCMG,AJAX na magari ya mizigo aina ya FAW ambazo kwa sasa magari hayo ya FAW yanatengenezwa Kibaha mkoani Pwani Pia GF imefungua ofisi katika mikoa ya Mwanza,Geita Morogoro na Songea ilikujiweka karibu na wateja alimaliza Smart.

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa akipata maelekezo kutoka kwa Afisa Masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd Smart Deus wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonyesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Chunya mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa akipokea zawadi ya vipeperushi na kalenda za kampuni yha GF Trucks & Equipment Ltd kutoka kwa Afisa Masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd, Smart Deus wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonyesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Chunya mkoani Mbeya.Kulia ni mkuu wa mkoa wa Mbeya Jumaa Homela