November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Mkuu Majaliwa aridhishwa na utendaji wa CPB,yenyewe yaahidi kuchapa kazi kwa ubora zaidi

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya

KUFUATIA kauli ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ya kuipongeza Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko (CPB) huku akisisitiza iendelee kutafuta masoko,bodi hiyo imesema imepata hamasa zaidi ya kuboresha na kutafuta masoko ya mazao ndani na nje ya nchi .

Hayo yamesemwa na Meneja wa CPB Fredy Mbilinyi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Katika maonyesho hayo Waziri Mkuu Majaliwa pamoja na kutembelea mambanda pia alitembelea banda la Bodi hiyo na kupata taarifa ya namna inavyofanya kazi ikiwa ni pamoja na kununua mazao ya wakulima,kuchakata na kuyafungasha na kutafuta masoko hatua ambayo ilimfanya waziri Mkuu Majaliwa kuridhishwa na utendaji wa Bodi hiyo na kuipongeza kwa kazi nzuri wanaiyoifanya ya kumgusa mkulima moja kwa moja.

Bidhaa za CPB zikiwa zimechakatwa na kufungashwa

Amesema wajasiriamali wanapaswa kutumia fursa ya kufanya kazi na bodi hiyo ili waweze kuboresha na kuongeza thamani ya bidhaa zao kabla hazijaingia sokoni.

Mbilinyi amesema wajasiriamali wenye nia ya kufanya kazi pamoja na wao wajitokeze ili bodi hiyo iingie mkataba nao wa kuboresha bidhaa zao kabla ya kuingia sokoni ili ziweze pata kirahisi masoko ya nje.

Mbilinyi amesema hivi sasa bodi hiyo imejipanga kuhakikisha inaendelea kutafuta masoko ndani na nje ya nchi ili wakulima waweze kupata soko la bidhaa zao kirahisi.

“Naomba wakulima ma wajasiriamali leteni bidhaa zenu tuziboreshe kabla hazijaingia sokoni,”amesema Mbilinyi.

Mbilinyi amesema  lengo lao kuona bidhaa za wakulima wa hapa nchini zinapata soko kubwa nje na ndani ya nchi bali na hilo ametoa wito kwa wakulima kuweza kuchangamkia fursa zinazotolewa na bodi hiyo ili waboreshe bidhaa zao kabla ya kuingia sokoni.