Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), amezindua rasmi Mfumo wa Kubadilishana Taarifa Serikalini (Government Enterprise Service Bus – GovESB) kwa kutumia kishkwambi, katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2025, katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Mfumo wa GovESB umesanifiwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao(e-GA) ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Tanzania Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan na Sheria ya Serikali Mtandao Namba 10, ya mwaka 2019, ya kuhakikisha mifumo yote ya taasisi za umma inasoma na kubadilishana taarifa, ili kuboresha huduma kwa wananchi.





More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi