May 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Mkuu atembelea Kituo cha Kuhifadhi Data Kimtandao NIDC.

Na Rose Itono,Timesmajira

SERIKALI imezitaka Taasisi za Umma na Binafsi kuwekeza katika Kituo Cha Kuhifadhi Data Kimtandao (NIDC) ili kupata huduma salama na kwa gharama nafuu

Akizungumza kwenye ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea Kituo cha Kuhifadhi Data kilichopo Kimtandao (NIDC) kilichopo Kijitonyama Dar es Salaam leo kwa lengo la kujionea namna Mfumo wa N- CARD unavyofanya kazi Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa alisema Taasisi za Umma na Binafsi hazina haja tena ya kuwekeza kwenye mifumo yao badala yake wakitumie Kituo Cha Kuhifadhi Data Kimtandao Kuhifadhi taarifa zao

“Lengo Kuu la Waziri Mkuu ambaye ameongozana na viongozi mbalimbali ni kishuhudia mafanikio makubwa yaliyopatikana
Kupitia Uwekezaji wa serikaliI katika TEHAMA,” amesema Silaa

Amesema kwa sasa serikali inaendelea na mchakato wa kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi kupitia Kadi Moja ya Jamii itakayounganishwa na taarifa zao za NIDA.

“Kadi hiyo itarahisisha miamala ya kifedha na itatumika katika huduma mbalimbali vikiwepo viingikii kwenye viwanja vya mpira, vivuko, usafiri wa mabasi yaendayo haraka (UDART), maarufu mwendo kasi, Taasisi za kifedha na maeneo mengine muhimu,”amesema Silaa.

Ameongeza kuwa mradi wa Digital Tanzania ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Kadi Jamii unaendelea kutekelezwa kwa lengo la kuhakikisha mifumo yote ya taasisi mbalimbali inasomana, ili kuwezesha utoaji wa huduma kwa ufanisi.

Amesema katika bajeti ya mwaka 2024/2025, serikali ilitenga Jumla ya Shilingi bilioni 10 kuiwezesha NIDC kuimarishaahuguli zake zikiwemo zinazotekelezwa kupitia mradi huo wa kidijitali.

“Kupitia mradi huu, wananchi wataweza kutumia Kadi Jamii yenye kuunganishwa na namba yao ya NIDA kufanya miamala yote ya kifedha na manunuzi, hivyo kuondoa hitaji la kubeba kadi nyingi,”ameongeza Silaa

Aidha amesema hatua hiyo inalenga kumrahisishia mwananchi maisha ya kila siku kwa kumuwezesha kutumia kadi moja tu kwa huduma mbalimbali, na kwamba serikali ipo kwenye mkakati wa kuhakikisha kila mwananchi anamiliki simu janja kwa gharama nafuu ili kuitumia sambamba na kadi hiyo.

Akizungumzia kuhusu Mkongo wa Taifa unaosimamiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) amesema tayari umeunganisha wilaya 109 kati ya 139 na baadhi ya nchi jirani za Afrika tayari zimeunganishwa na mkongo huo hatua ambayo itaongeza ufanisi na kupanua huduma za kidijitali nchini.