March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Mkuu atembelea Banda la Yas maonesho ya Nanenane 2025

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametembelea Banda la Yas kwenye Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima maarufu (Nane Nane) yanayoendelea jijini Dodoma.

Maonesho hayo ya Kitaifa ya Wakulima maarufu (Nane Nane) yanaendelea jijini Dodoma ni uthibitisho kuwa Yas na Mixx ni mshirika wa maendeleo kwa wakulima na watanzania kwa ujumla.

Lakini pia, kwa kutoa suluhisho rahisi, salama na jumuishi katika mawasiliano na miamala ya kifedha.

“Tunayo furaha kubwa kutembelewa na viongozi, wageni na wadau mbalimbali kwenye banda letu katika maonesho ya Nanenane 2025, akiwemo Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa,”.

Mara baada ya kutembelea Babda hilo, Waziri Mkuu alipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mixx by Yas Kanda ya kati, Charles Gasper.

Yas na Mixx, zimejipambanua kuwa mshirika wa maendeleo kwa wakulima na wananchi kwa ujumla kwa kutoa suluhisho rahisi, salama na jumuishi katika mawasiliano na miamala ya kifedha.

“Yas tupo na wakulima kwenye safari yao ya mafanikio,”.