Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, IRINGA
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, ameshangazwa kupatiwa taarifa za ujenzi wa nyumba za walimu wa shule ya sekondari ya Iramba Wilaya Mufindi mkoani Iringa kujengwa kwa Sh milioni 100 na kuagiza kufanyika upya mapito ya gharama hizo.
Majaliwa ameyasema hayo leo akiwa mkoani Iringa kwa ajili ya ziara akiwa anazindua shule ya sekondari ya wasichana ya Iramba.
“Makadirio ya fedha inayokuja mnataka kujenga nyumba tano kwa Sh milioni 500 mwalimu hakuna nyumba ya Sh milioni 100 kwa mwalimu mmoja,”amesema Majaliwa.
“Nyumba za walimu mmoja ni Sh. milioni 25 hadi 30 na tumejenga zipo hizo nyumba hiyo ni nyumba yenye vyumba vitatu, choo na eneo la stoo na kila kitu na ramani zipo nyie mnataka kujenga kwa ramani zipi,”alihoji
Majaliwa alimtaka Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia jambo hilo hata kama wanata kujenga jengo kubwa yenye kuishi walimu wawili haifiki Sh milioni 60.
“Lakini nyie mmekadiria Sh milioni 100 hizi nyingi mfanye mapitio tena nisisikie mmejenga nyumba kwa Sh milioni 100 labda kama nyumba hizo ni nne kwa wakati mmoja. Mhandisi pitia tena hesabu zenu na kuhakikiwa na kamati ya elimu ya Halmashauri,”amesema Majaliwa.
More Stories
Serikali ya Kijiji Ilungu yawakatia bima za afya wananchi 1500
TMA kuendelea kufuatilia mifumo yake
Wassira:Waliopora ardhi za vijiji warudishe kwa wananchi