December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama

Waziri Mhagama :Msiwatumie wanawake kama mawakala wa kuleta vurugu

Na Doreen Aloyce, TimesMajira Online, Dodoma

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama amevitaka vyama vya siasa nchini kutowatumia wanawake kama mawakala wa kuleta vuruga katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu badala yake wawaache wakishiriki kwenye uchaguzi huo.

Kuwa kipaumbele cha Rais John Magufuli katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba,mwaka huu,unakuwa wa huru,amani na na haki.

Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na viongozi 15 wa vyama cha siasa katika kuelekea uchaguzi mkuu.

Amesema kuwa amani inapotoweka waathirika wakubwa ni wanawake,watoto na wazee hivyo na kuwawihi vyama kutokuwatumia na kuwafanya mawakala wa vurugu kwani mwanamke anapaswa kuwa Balozi wa Amani .

“Naomba vyama cha siasa muwaache wanawake wakishiriki uchaguzi na sio kwa vurugu niwasihi wanawake muwe mabalozi wema katika kutoa elimu kwa wanawake wengine mshikamano uwe nguzo yenu kuleta ushindi na msikubali kutumika kubomoana katika vyama bali ajenda yenu kubwa iwe kukataa ukabila,udini na ubaguzi.”

“Niwatake wanawake kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya rushwa kiu yangu ni kuona sio wahanga na hata ikitokea wasizidi wawili tukipinga kwa nguvu zote itasaidia Taifa letu kuwa huru “amesema Mhagama.

Naye Msajili wa vyama cha siasa Jaji Fransic Mutungi amesema kuwa vyama vyote hakuna sababu ya kupoteza Amani ya Taifa katika Uchaguzi bali unapaswa kumalizika kwa Amani jambo ambalo litaleta sifa kwa nchi huku akidai kwamba maendeleo hayana chama.

Queen Sendiga ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),alisema lengo la mkutano huo ,viongozi wa mbambali wanawake wa vyama vya siasa kumshukuru na kumpa zawadi Waziri Jenesta Mhagama kwa kazi aliyoifanya kwenye sSrikali ikiwemo wizara yake kusimamia na kushughulika vyema masuala yanayohusiana na vyama cha siasa.

“Tumeamua kumpongeza Waziri Jenesta baada ya kutambua na kumtathimini kazi kubwa aliyoifanya ndani ya kipindi cha miaka mitano huku tukimtakia kila la heri katika kugombea tena”alisema Queen.

Naye Abdul Mluya ambaye ni katibu Mkuu Chama cha Democratic Party (DP) amesema kuwa chama kina mpango wa kumsimamisha mgombea urais wa kupeperusha bendera ya chama ambapo amesema kuwa Serikali kupitia kauli ya Rais Magufuli isimamie uchaguzi uwe wa huru na haki huku tume ikipeleka watu wenye uadilifu ambao wataisimamia uchaguzi huo.