January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Mchengerwa atoa maagizo DART, UDART

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesisitiza watumishi wa DART pamoja na watoa huduma wake kuhakikisha wanafanya kazi kwa ushirikiano katika kutoa huduma bora kwa wananchi na kujibu hoja za abiria kwenye Mradi wa DART.

Alitoa agizo hilo jana Septemba 2, 2024 wakati akizindua Kadi Janja na Mageti janja kwa ajili ya kununua na kuhakiki tiketi za usafiri wa Mabasi Yaendayo haraka katika
Kituo Kikuu cha Kimara Jijini Dar es Salaam

Mchengerwa amesema kumekuwa na baadhi ya madereva wa mabasi yaendayo haraka wanatumia kauli sizizofaa kwa abiria hali inayoleta changamoto kwa wananchi wanatumia usafiri huo.

Kadhalika, Waziri Mchengerwa amesema kuwa mbali na kuwarahishia abiria kusafiri kwa wakati pia matumizi ya Kadi pamoja na mageti janja vitasaidia mradi kati katika utunzaji wa mazingira.

KWaziri Mchengerwa amesema mfumo huo wa ukataji tiketi janja utasaidia kuondoa udanganyifu kwenye mapato, kuokoa muda , kutunza mazingira ukilinganisha na awali walipokuwa wakitumia tiketi za karatasi huku akisema dhamira ya serikali ni kutibu hoja za wananchi za mda mrefu

Aidha amesema kutumia kadi janja hizo ni kuendana na teknolojia ya kiwango cha juu na mapinduzi makubwa ya kuwahudumia watanzania wa Mkoa wa Dar es salaam

Huku MChengerwa akiwataka wakala wa mabasi hayo kabla ya Disemba mwaka huu Mkoa wa Dar es salaam uwe na mabasi ya kutosha yatakayokidhi huduma za wananchi wa Mkoa huo .

Aidha Waziri Mchengerwa aliupongeza
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Kamati ya Bunge kuhusu kuachana na tiketi za Karatasi.

“Dhamira ya Mheshimiwa Rais ni kuhakikisha tumeboresha usafiri wa Umma katika Jiji la Dar es Salaam kwa kumaliza changamoto zote za abiria kabla ya kwenda kwenye mikoa mingine” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa mabasi yaendayo haraka (DART)Dk. Othuman Kihamia amesema mfumo wa ukataji tiketi kwa kutumia kadi janja utasaidia kuondoa matumizi ya katasi na kuchafua mazingira,Usumbufu wa chenchi, pamoja na kupunguza foleni wakati wa ukataji wa tiketi.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa DART, Dkt. Florens Turuka amesema kwa DART ni jambo la fahari kuona mifumo inaimarika kwenye kuendesha usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka na dhamira yao ni kuona kuwa mifumo hit inarahisisha na kuleta tija Jijini Da es Salaam.

Kadi na Mageti janja yaliyozinduliwa yanayotokana na Mfumo wa
Serikali wa Ukusanyaji nauli (AFCS) ni juhudi za serikali katika kutumia wataalam wa ndani kunda mifumo itakayotoa suluhu ya
changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika kuzifikia
huduma.