Na David John,TimesMajira online, Dar
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohamed Mchengerwa amezitaka wizara, idara na taasisi za Serikali kuhakikisha zinapitisha viongozi wake katika mafunzo yanayoandaliwa na kutolewa na Taasisi ya UONGOZI.
Mchengerwa ameyasema hayo jana wakati wa ziara yake katika taasisi hiyo ambapo amesema taasisi zote hapa nchini ambazo zina watumishi wa umma wajipange, watenge bajeti zao kuhakikisha kwamba wanapita kwenye taasisi hii ili tuweze kupikwa zaidi.
“Na wale ambao tunaamini wanaweza kutusaidia, tuwatumie.Tunao wakuu wa mikoa ambao wana uzoefu zaidi, waiteni na kuwatumia ili kuendelea kutoa elimu.
“Wakuu wa mikoa na Wilaya ambao ni vijana na pengine wanadhani wao wakishateuliwa ndiyo wameshamaliza, kwamba hakuna mamlaka ya kuwachunguza na kuwafuatilia, ni lazima tuzingatie sana,” amesema Waziri.
Aidha,Waziri Mchengerwa ametoa msisitizo kuhusu suala la utendaji kazi kwa wizara, idara na taasisi zote za serikali; ikiwemo kuhakikisha kwamba stahiki za watumishi wa umma zinapatikana kwa wakati na kwa mujibu wa sheria, kuhakikisha watumishi wanaokaimu nafasi mbalimbali kwa muda mrefu waweze kuthibitishwa katika nafasi hizo.
Endapo wana sifa zinazostahili, na kuhakikisha maadili na taratibu za utumishi wa umma zinazingatiwa ili kuleta ufanisi katika kazi na huduma zitolewazo kwa wananchi.
More Stories
CPA.Makalla :CCM kutumia 4R za Rais Samia katika uchaguzi Serikali za Mitaa
CCM kutumia 4R za Samia Uchaguzi Serikali za Mitaa
Dkt. Mpango awasilisha salam za Rais Samia mazisha Baba yake mzazi, Gavana Tutuba