Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameongoza sehemu ya kwanza ya Kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Nordic na Afrika Mei 3, 2024 ikiwa ni siku ya pili na ya mwisho ya kikao hicho.
Mawaziri hao waliokutana jijini Copenhagen nchini Denmark wametoa hoja mbalimbali za kukuza ushirikiano kati ya nchi za Afrika na za Nodric pamoja na kuimarisha mwelekeo wa vikao vijavyo vya Nordic ikiwa ni pamoja na kuwa na viongozi wa muda.
Kutokana na kuwa masuala mengi yanayojadiliwa kuwa ni ya kiuchumi na uwekezaji, imependekezwa kuwa pengine upo umuhimu wa kuanzishwa kwa Mkutano wa Mawaziri wa sekta hizo wa Nchi za Afrika na Nordic ili kurahisisha utekelezwaji wa yale yanayoafikiwa.
Msisitizo mkubwa katika mkutano huu umehimiza kuwepo kwa sauti ya pamoja katika masuala ya kimataifa, kutumia vyema nguvu-kazi vijana katika mipango ya mbeleni, kuhamasisha na kulinda amani duniani kote.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu