December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Makamba aguswa wanawake kujifungulia gizani Geita

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Nishati Januari Makamba ameelekeza wataalam wa Shirika la Umeme nchini(Tanesco) pamoja na wakandarasi Julai 16,2021 kufika katika Kata ya Buleba Halmashauri ya Mji wa Geita kufanya upembuzi yakinifu Ili wapeleke umeme kwenye Zahanati ya Bulela ambako imebainika wanawake wajawazito wanajifungulia gizani.

Makamba ametoa maelekezo hayo Julai 14 ,2022 akizungumza na wananchi wa Kata hiyo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa Diwani wa Kata hiyo Salome Kitula akieleza kuwa katika Zahanati hiyo hakuna Umeme na kusababisha mama wajawazito kujifungulia gizani au kutumia mwanga Simu.

Aidha nishati mbadala ya Mionzi ya Jua(Solar) iliyokuwa inatumika kwenye Zahanati hiyo imeharibika kwa muda sasa,hali inayosababisha kutokuwa na nishati yoyote inayowezesha mwanga wakati wa usiku.

Pia Makamba ameaahidi kuitengeneza solar iliyoharibika katika Zahanati hiyo ili iendelee kutumika wakati serikali ikiendelea na mchakato wa kupeleka umeme katika Zahanati hiyo.