December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Kairuki akutana na mamlaka wa uholanzi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Taifa kuhusu Utekelezaji wa Nchi katika Jukwaa la Kizazi chenye Usawa, Mhe Angellah Kairuki, amekutana na kufanya mazungumzo na Malkia wa Uholanzi, Mhe. Maxima ambaye pia ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala va Mfumo Jumuishi wa Fedha.

Mazungumzo hayo yamefanyika tarehe 19 Oktoba 2022 na yalilenga kujadili masuala ya Huduma za Kifedha Jumuishi Nchini Tanzania.

Aidha, Katika Mkutano huo wa mazungumzo Waziri Kairuki aliambatana na Wajumbe wengine wa Kamati Ya GEF Tanzania.