Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema wakulima wanatakiwa kuhamasishwa kujikita na kufuata maelekezo ya kilimo cha kisasa.
Wito huo umetolewa leo jijini Mwanza na Waziri Hasunga wakati wa mkutano maalumu wa wadau wa tasnia ya pamba wenye Kauli Mbiu isemayo zalisha pamba kwa tija na ubora kuongeza kipato na kufikia uchumi wa viwanda.
Hasunga amesema, wakulima wanapaswa kuhamasishwa kwenye kilimo cha kisasa ili kuongeza uzalishaji kwa kutumia pembejeo bora ikiwemo mbegu na viuatilifu zinazoongeza uzalishaji pamoja na teknolojia ya kisasa ambayo mkulima ataweza kupata kilo 1,350 kwa hekari moja kama nchi nyingine zinazolima pamba .
Anesema ifike mahali zao la pamba liwe linachakatwa ndani ya nchi kwa kuhakikisha viwanda vinafufuliwa na watu wanawekeza ili kuwe na uhakika wa soko.
“Asilimia 65 ya viwanda vinategemea malighafi kutoka kwenye kilimo, hivyo lazima tuwezeshe mfumo wa kilimo wa kisasa, kwani kilimo ndio kinatupatia asilimia 100 ya chakula,” amesema Waziri Hasunga.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best