January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Gwajima kushirikiana na wadau wa kupambana na ukatili kuboresha teknolojia ya kidijitali

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kupambana na ukatili wanatarajia kutenga wiki maalumu ya kujadili na kuboresha teknolojia ya kidijitali na kuongeza ubunifu kwa lengo la kuwafikia kirahisi wananchi wanaofanyiwa ukatili.

Hayo ameyasema leo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Dk. Dorothy Gwajima alipotembelea Shirika la Kupambana na Ukatili Kidijitali

“Tunakuja na mkakati wa kuinua huduma ya kidijatali ili ifike hata vijiini kutakuwa na kikao kikubwa cha wadau itakuwa ni wiki ya ubunifu na kuweka suluhu ili jamii ielewe na kuchukua hatua.

“Tutengeneze simu za watoto zenye Programu za watoto uwe ni ulimwengu wa watoto tu lazima tuende huko, tuweke nguvu huko hiyo itamuepusha mtoto na mambo mabaya tuje tupate wafadhiri twende huko “alisema.

Mbali na hayo Waziri Gwajima amesema wabunifu wa teknolojia za kidijitali waje na simu zenye Programu Maalumu kwaajili ya matumizi ya watoto ili kuwaepusha kutumuia simu za watu wazima ambazo baadhi yake hutumika kuporomosha maadili kwa watoto kwa kuangalia vitu visivyofaa.

Aidha Dk. Gwajima aliwataka wadau wa kupambana na ukatili wanaoshughurika na masuala ya kidijitali kufanya uratibu wa pamoja ili kuona namna ya kukamilisha shughuli hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Tangible Intiative Development alimpongeza Waziri Gwajima kwa kuwatembelea na kutambua umuhimu wa huduma ya Teknolojia ya Kidijtali katika mapambano ya ukatili.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa wabunifu wao wamekuwa siyo tu sehemu ya kuisaidia jamii ya kitanzania lakini teknolojia hizi kwa nchi zingine wamekuwa wakizihitaji na kuzitumia

Amesema Waziri Gwajima amewaahidi kuwaratibu vyema na kuwasaidia kutambulika zaidi katika jamii.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Dk. Dorothy Gwajima Shirika la Kupambana na Ukatili Kidijitali (TIFLD) katika muendelezo wa siku ya wanawake duniani ambapo ameshuhudia bunifu mbalimbali za teknolojia ya mawasiliano zinavyofanya kazi kumsaidia mwanamke katika maeneo mbalimbali.
Afisa Teknolojia ya Mawasiliano kutoka Shirika la Amref Health Africa, Ezra Mfaume akimpa maelezo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu Dkt. Doroth Gwajima namna mfumo wa LEAP unavyofanya kazi wakati Waziri alipotembelea maonesho yaliyoandaliwa na Muungano wa Asasi za Kiraia (Mkuki coalition) katika muendelezo wa siku ya wanawake duniani ambapo ameshuhudia bunifu mbalimbali za teknolojia ya mawasiliano zinavyofanya kazi kumsaidia mwanamke katika maeneo mbalimbali.