December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Gwajima aandaa tuzo kwaajili ya Mtaa wa Amani Kipunguni

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi Maalum Dkt, Dorothy Ngwajima,amesema MTAA wa AMANI Kata ya Kipunguni anaandaa tuzo Maalum kwa ajili ya Mtaa AMANI.

Waziri Dkt,Dorothy Ngwajima alisema hayo katika ziara yake kukagua maenesho na kazi za Mikono zinazofanywa na Sauti ya Jamii katika wiki ya madhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

“Ninawapongeza viongozi wa Mtaa wa Amani kata ya Kipunguni ,Mtaa wa Amani ni Mtaa wa darasa la kujifunza kwa TANZANIA wamefanya kitu kikubwa kuanzisha SAUTI ya Jamii kumshughulikia maswala ya ukatili Wizara yangu itaweka kambi kujifunza pamoja na kuwapa tuzo ya Wizara kwa ubunifu wao” alisema Dkt , Ngwajima.

Dkt, Dorothy Ngwajima alisema atawaleta wataalam wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kurekodi dokomentary na kujifunza .

Aidha alisema Wenyeviti wa Serikali za mitaa ni chanzo cha Ustawi wa Jamii amewataka wabuni vitu vya kupinga ukatili kwa ajili ya kusaidia Jamii kupinga vitendo hivyo.

Waziri Dkt, Ngwajima aliwataka wanaume kuunga mkono juhudi za Sauti ya Jamii Kipunguni

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija alisema maswala ya ukatili ya kijinsia Wananchi wa Wilaya ya Ilala wanapewa Elimu ya kutosha matukio ya kijinsia .

Alisema yakitokea matukio hayo wanayapatia ufumbuzi wake kupitia madawati ya jinsia Wilaya ya Ilala.


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kipunguni Daniel Malagashimba aliwataka Maafisa Ustawi wa Jamii washirikiane na Wenyeviti wa Serikali za mitaa katika maswala ya ukatili wa kijinsia.

Malagashimba alisema Wenyeviti wa Serikali za mitaa wanateleleza Ilani ya chama Cha Mapinduzi CCM kwa ajili ya kuisaidia Serikali kutatua changamoto wanazofanyiwa Wana Jamii.