Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana Julai 10, 2023 ametembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ambapo ameshuhudia Taasisi za wizara hiyo zikitoa huduma kwa wananchi.
Akiwa katika Banda hilo, ameshuhudia michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa Draft, Netiboli pamoja na kazi zinazofanywa na Wadau wa Wizara hiyo wakiwemo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Sanaa za Ufundi na uchoraji.
Aidha, ameshuhudia Sanaa ya jukwani kutoka kwa waimbaji Chipukizi ambao wamepatikana kupitia shindano lilioandaliwa Wizara kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) katika maonesho hayo pamoja na burudani ya Msanii wa Taarabu Isha Mashauzi.
Aidha, Chana amepata nafasi ya kutembelea mabanda mengine ikiwemo Banda la Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Tigo, Vodacom pamoja pamoja na Azam.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja