January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Chana aendelea kukaribisha wawekezaji kwenye sekta ya Utalii

Na Penina Malundo, TimesMajira, Online

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa China na wenye asili ya Kiasia waishio nchini Tanzania wakiongozwa na Xian Ding na Mtendaji Mkuu na   Gregory Hess ambaye  Mwanzilishi wa Kampuni ya Tree GLOBAL yenye makao makuu yake nchini Uswisi.

Katika vikao vyake na wawekezaji hao leo,Waziri Chana aliwapongeza kwa kuonesha nia ya kuwekeza nchini akieleza kuwa hayo ni matokeo chanya ya juhudi za Rais wa  Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia pamoja na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji.

Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii  ipo tayari kutoa ushirikiano unao hitajika  kwa mwekezaji yeyote mwenye nia njema ya kuwekeza Tanzania.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu na Mwanzilishi wa Kampuni ya Tree GLOBALGregory Hess amemweleza Waziri Chana kuwa  Kampuni yake inawekeza kwa kurejesha mazingira katika hali ya awali ili kupambana na adhari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi.