Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Ngara-Kagera
Kufuatia Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kumuagiza Waziri wa Maji “kufika Ngara kujiridhisha juu ya utekelezaji wa mradi wa maji unaondelea pamoja na kuweka mipango ya ukamilishaji”. Waziri Aweso ametekeleza agizo leo tarehe 24 Februari ikiwa ni Siku mbili tu zimepita tangu Rais alipofika Wilayani Ngara.
Katika kukamilisha Mradi huo, Aweso amemuelekeza Mkandarasi NYAMAKA CO. LTD anayechimba kisima hicho kukamilisha Kazi hiyo kwa haraka ili usanifu wa Miundombinu ya Maji iweze kuanza na hatimae kujengwa kwa mradi.
Aidha, Waziri Aweso amebainisha kwamba, Mahitaji ya Maji katika Mji wa Ngara kwa sasa ni Lita MILIONI 2.8 uzalishaji kwa visima vitatu vilivyopo kwa sasa LITA MILIONI 1.5 ujanzo wa matanki yaliyopo ni LITA LAKI SITA TISINI NA SITA( 696) kwa mwaka 2021/22 serikali imetenga Tsh 793,585,934.45 kwa ajili ya uchimbaji kisima kirefu,ujenzi wa mtandao na ukarabati wa miundombinu ya maji.
Wizara imechimba kisima kipya ambacho kinauwezo wa kuzalisha Maji Lita 50,000 kwa Saa sawa na MILIONI MOJA kwa Siku. Kisima hicho kitaongeza uzalishaji wa Maji na kufikia Lita MILIONI 2.5 kwa Siku.
Tayari Wizara imepeleka Shilingi milioni 100 ambazo zimetumika kutafiti na Kuchimba kisima kipya.
More Stories
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25