December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Aweso amtaka Mkandarasi kuongeza nguvu kazi mradi wa chanzo cha maji Butimba

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

Waziri wa Maji Juma Aweso ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa chanzo kipya cha maji Butimba huku akimtaka Mkandarasi kuongeza nguvu kazi Ili aweze kukamilika mradi huo kwa wakati ifikapo Februari 2023.

Huku akitahadahrisha kuwa wakiona Mkandarasi anatekeleza mradi kinyume na mkataba wataachana naye na kuweka mtu mwingine ambaye atafanya kazi kwa wakati na wananchi wapate maji.

Waziri Aweso ameyasema hayo wakati alipotembelea mradi huo akiwa ameongozana na Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mwanza (MWAUWASA),ambapo ameelezaka kuwa mradi huo Wizara kwao ni WA kimkakati ambao unaenda kutatua changamoto ya maji katika maeneo mengi ya Jiji la Mwanza.

Hivyo wamepanga itakapofika Februari mwakani Mkandarasi awakabidhi mradi huo Ili wananchi wa Jiji la Mwanza waendelee kunufaika na kazi nzuri ya Rais wao hivyo michakato ambayo haina ulazima katika utekelezaji wa mradi huo hawawezi kukubaliana nayo.

Ameeleza kuwa,mahitaji ya maji ni zaidi ya lita 160,lakini uzalishaji wa maji kupitia mitambo iliopo ni lita milioni 90,wameona uhitaji mkubwa na ongezeko kubwa la watu la Jiji la Mwanza pia wabunge wa Jiji hilo wamekuwa wakipiga sana kelele kwa sababu ya maji,waamshukuru Rais wamepata fedha zaidi ya bilioni 69.kwa ajili ya kuongeza chanjo kipya cha maji Butimba ambacho kitazalisha lita milioni 48 ambayo yatakwenda kuongeza uzalishaji Ili wananchi wa Nyamagana na Ilemela waweze kupata huduma ya maji safi na salama.

“Nimefika na nimeridhishwa na kazi ambayo inatekelezwa ambapo imefikia asilimia 35, lakini tumetoa maelekezo mahususi kwa Mkandarasi wa mradi huu,kuwa hana kisingizio cha fedha kwa sababu utekelezaji wa mradi wa maji inategemea na fedha,fedha ipo kwaio hatekeleze kwa maana ya kuongeza nguvu kazi ili kuhakikisha kazi inakamilika kwa mujibu wa mkataba na kuzingatia ubora,”ameeleza Aweso na kuongeza kuwa

Sanjari na hayo Waziri Aweso amefafanua kuwa kuhusu upatikanaji wa maji kwa maeneo ya mjini na vijijini wamewekewa mkakati mahususi itakapofika 2025 asilimia 85 ya upatikanaji wa maji vijijini na asilimia 95 mjini.

Ameeleza kuwa vijijini kwa sasa wana asilimia 74 ya utekelezaji wa miradi ya maji na mjini ni asilimia 86 ya kuhakikisha watu wanapata huduma ya maji safi na salama lakini wana miradi ya kimkakati ya kuhakikisha wanafukia asilimia hiyo.

“Vijijini sasa hivi tunatekeleza miradi 1029 ambayo ipo katika hatua mbalimbali ya utekelezaji wake ambayo kukamilika kwake kutaongeza upatikanaji wa huduma ya maji na mjini tumesaini miradi ya miji 28 ambayo ni miradi ya kimkakati itatumia vyanzo vikubwa vya maji kwa maana ya maziwa na mito yenye gharama ya zaidi ya tirioni 1 ambazo zimewekezwa kuhakikisha watu wanapata maji safi na salama,”ameeleza Aweso.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MWAUWASA Mhandisi Leonard Msenyele, ameeleza mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita za maji milioni 48 kwa siku kwa thamani ya bilioni 69 ambapo chanzo kizima kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 160 lakini wameanza na awamu ya kwanza ya mradi wenye uwezo wa kuzalisha lita za maji milioni 48.

“Hatuna changamoto katika suala la malipo Mkandarasi analipwa kwa wakati,mradi ulianza utekelezaji wake Februari 2021 na inajengwa kwa mfumo wa kusanifu na kujenga,na tunategemea ukamilike Februari 2023, sasa hivi umefikia asilimia 35, lengo ni kuhakikisha tunaongeza uzalishaji wa maji kwa Jiji la Mwanza Ili kuondoa changamoto ya upungufu uliopo,”ameeleza Mhandisi Leonard.

Naye Mjumbe wa Bodi ya MWAUWASA Dkt.Elibarik Mmari,ameeleza kuwa mradi huo awamu wa kwanza utaweza kuzalisha lita za maji milioni 48 bado kuna awamu tatu ambazo zitajengwa baadae kwaio wanafikiri ukikamikika utapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya maji.

“Namuomba Waziri katika Wizara yako uone kwa namna gani utatafuta fedha ili kumalizia awamu zilizobakia eneo la mradi huu ili kuweza kuondoa au kupunguza changamoto ya maji kwa sababu hapa tutapata lita milioni 48 ukijumlisha na zilizopo lita milioni 90 tutakuwa na lita milioni 138 hivyo upungufu bado utakuwepo,”ameeleza Dkt.Mmari.

Waziri wa Maji Juma Aweso alisikiliza maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa MWAUWASA Mhandisi Leonard Msenyele, wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa chanzo cha maji Butimba ambapo aliongozana na Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mwanza (MWAUWASA).(Picha na Judith Ferdinand)
Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa chanzo cha maji Butimba ambapo aliongozana na Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mwanza (MWAUWASA).(Picha na Judith Ferdinand)
Mkurugenzi wa MWAUWASA Mhandisi Leonard Msenyele, akizungumza wakati Waziri wa Maji Juma Aweso wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa chanzo cha maji Butimba ambapo aliongozana na Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mwanza (MWAUWASA).(Picha na Judith Ferdinand)
Mjumbe wa Bodi ya MWAUWASA Dkt.Elibarik Mmari akizungumza wakati Waziri wa Maji Juma Aweso wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa chanzo cha maji Butimba ambapo aliongozana na Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mwanza (MWAUWASA).(Picha na Judith Ferdinand)
Muonekano wa mradi wa ujenzi wa chanzo cha maji Butimba ulivyofikia utekelezaji wake kwa asilimia 35.(Picha na Judith Ferdinand)