January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Ashatu: Wizara itaendeleza jitihada zilizopo kuleta matokeo chanya

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imesema itaendeleza jtihada zilizopo na kuziboresha ili kuiletea nchi matokeo yaliyokusudiwa hususani katika kuongeza uwekezaji, kuongeza mauzo nje, kutoa fursa zaidi za ajira na kuongeza mchango wa Sekta katika Pato la Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari Jana jijini Dar wakati akielezea mafanikio ya mwaka mmoja wa serikali ya awamu ya Sita, Waziri wa uwekezaji, viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji alisema wanaendelea kuwa na imani na mazingira bora ya biashara ndani ya Taifa letu, Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikifanya makongamano mbalimbali ya Biashara na Uwekezaji ambapo Yapo makongamano yaliyofanyika ndani ya nchi yetu na nje ya nchi yetu;

” Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Kenya (06/05/2021), Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Burundi (18/07/202 1), Kongamano la Wadau wa Sekta ya Alizeti pamoja na maony3sho ya Biashara (10-15/08/2021), kongamano la Biashara kati ya Tanzani na Uingereza (16/11/2021), Kongamano la Biashara na Uwekezaji kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Taifa letu (08/12/2021), Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa (14/02/2022), Kongamano la Biashara na Uwekezaji, kati ya Tanzania na Ubelgiji (17/02/2022), na Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu(27/02/2022); “

Ashatu alisema Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi makini wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Tanzania imefanikiwa kuendeleza utekelezaji wa sera na mikakati ya ujumla ya maendeleo ya Nchi ili kuhakikisha kuwa Nchi yetu inatekeleza majukumu ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kama yalivyoainishwa kwenye mipango na mwelekeo wa Nchi yetu kiuchumi.

Aidha Waziri Ashatu aliyataja mafanikio ya makongamano hayo yakiwemo;

“Upatikanaji wa vibali vya kazi, mafanikio katika uwekezaji, upatikanaji wa ardhi ya uwekezaji, utengenezaji wa dirisha moja la uwekezaji, Kukamilika kwa Mwongozo wa Uwekezaji kupitia Kitabu cha Pamoja cha miradi ya uwekezaji, uanzishaji wa kongano za viwanda, uendelezaji wa ujenzi wa kongano ya viwanda Kwala Pwani, Kuimarisha Majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi n.k”

Mbali na hayo Waziri Ashatu alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu pia imewezesha uhumizaji wa Mafunzo kwa Wajasiriamali ambapo kupitia maelekezo yake jumla ya Wajasiriamali 4,156 (wanaume 1,662 wanawake 2,494) wamepatiwa ujuzi na mafunzo katika nyanja za Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara na Usindikaji wa mazao ya kilimo, mifugo, misitu na madini.

Waziri Ashatu alisema wanaendelea na wataendelea kujenga mazingira bora, rafiki na wezeshi kupitia mapitio ya sera, mikakati na sheria mbalimbali; kutunga sera mpya na kutekeleza Mpango Kazi wa Blueprint lakini pia Ushirikishaji wa Sekta Binafsi utaendelea kupewa msukumo wa kipekee.