December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wazee Kyela wamuomba Mbunge awaombee posho

Na Esther Macha Timesmajira, Online Kyela

BAADHI ya wazee wa Halmashauri. Ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, wamemuomba Mbunge wa Jimbo lao Ally Mlaghila kuwaombea posho za uzeeni ili waachane na utegemezi kutoka kwa ndugu na jamaa zao.

Akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake,wakati wa mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo hilo amesema wazee hawana uwezo wa kuzalisha mali wala kuchangia uchumi, hivyo ni vyema serikali ikaangalia namna ya kuwapa posho angalau ya kukidhi mahitaji yao.

Mwafulila amesema kwa kuwa Mbunge wao ni mwakilishi wa wananchi na wamemuamini hivyo ana nafasi ya kuwasemea kupitia jukwaa la Bunge kwenye mamlaka husika.

“Sisi tumekuchagua wewe ili uende Bungeni ukatusaidie kutuombea posho ya kifuta jasho cha kuzeeka kwani tumesaidia sana taifa hili,”amesema Mzee huyo.

Naye Atupele Mwakipesile ambaye ni mzee amesema kuwa hospitali ya Ipinda imekuwa ikiwatesa wazee hivyo ni bora igeuke kuwa sekondari na shule za msingi kuliko kuwa hospitali maana wakati wa matibabu madaktari hawawajali kabisa.

“Hii hospitali ni bora kugeuka kuwa sekondari na shule za msingi umuhimu wa kuwa hospitali haupo kabisa sababu wewe ni Mbunge wanakufahamu watakukimbilia na kukupa huduma ila sisi wazee ambao ni walala hoi hawana muda na sisi tunaomba utusaidie sisi wazee,”amesema mzee huyo.

Akiwa Kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero Mbunge wa Jimbo la Kyela Ali Mlagila kwa unyenyekevu amekiri kuchaguliwa ili atumwe kuwakilisha hoja zao na hilo ambelibeba kwa uzito wake atalifikisha bungeni kikao kijach

Mlaghila amesema suala la manyanyaso amelikemea sana kuna kipindi iliwahi kutokea ambapo wauguzi wamekuwa na tabia ya kunyanyasa akina mama na wagonjwa wengine.

“Nimeambiwa hospitali ya Ipinda wananyanyasa wagonjwa nipeni muda usiku wa leo nilifatilie tena nilijua limeisha,kesho namleta mganga aje alijibie hili suala mtasikia wenyewe wananchi tujitahidi kufika kumsikiliza ili tupate ufumbuzi wa kero zenu hususani hili la wazee wetu,”amesema Mlaghila.