Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online,Nkasi
Ofisa Ustawi wa Jamii wilayani Nkasi mkoani Rukwa,Oscar Mdenye, amewaonya Wazazi wanaowatumia watoto wao kufanya biashara za kuuza miwa katika stand kuu ya Namanyere muda ambao walitakiwa wawepo shule.
Onyo hilo limetolewa, baada ya kubainika kuwepo kwa watoto ambao ni wanafunzi, muda wanaopaswa kuwa shuleni wakiwa wameambatana na wazazi wao kwenye biashara mbalimbali ikiwemo ya miwa mjini Namanyere.Hali ambayo ufanya watoto hao kukosa haki ya kupata elimu.
Sambamba na hilo,Oscar amewaonya wamiliki wa vibanda vya kuchezesha ‘game’ kwenye ‘computer’,kutoruhusu watoto kucheza michezo hiyo muda wa shule.Atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.
Amefafanua kuwa, hivi sasa imebainika kuwa watoto wengi majira ya asubuhi ukimbilia kujificha kwenye michezo hiyo ya ‘game’,badala ya kwenda shuleni.Na wakati mwingine ulazimika kuiba fedha za wazazi wao na kwenda kucheza michezo hiyo.
Amedai kuwa kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wazazi juu ya watoto wao ambao wengi wao hawaonekani nyumbani, huku muda mwingi wanakuwepo kwenye vibanda vya ‘Computer’,ambavyo wanacheza ‘game’hadi majira ya usiku.Hali iliyochangia watoto wengi wanaoshinda kwenye michezo hiyo wameshuka kitaaluma.
Mdenye amesema kwa mujibu wa sheria ya mtoto ya mwaka 2009,inafafanua kuwa jukumu lote la malezi ya mtoto ni la wazazi ama walezi na kukidhi mahitaji yao yote.Na siyo kumtumia mtoto kibiashara kwa lengo la kutafuta kipato ni kwenda kinyume na sheria za nchi.
Baadhi ya Wananchi waliozungumza na Timesmajira Online, wamepongeza hatua hiyo iliyochukuliwa na serikali juu ya suala hilo,hivyo watakua mstari wa mbele katika kutoa taarifa pale wanapoona sheria inakiukwa kwa watoto kuwatumikisha wenye shughuli za kiuchumi muda wa shule.
Maria Mbalazi mkazi wa Kijiji cpha Mkole ameeleza kuwa,moja ya jukumu la wazazi ni kuhakikisha watoto wao wanapata huduma zote za msingi.Huku kutafuta kipato cha familia ni jukumu la mzazi.
“Kuwapa majukumu ya utafutaji kipato watoto tena muda wa kuwa shule ni kuwanyima haki zao muhimu wanazotakiwa kuzipata,”.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best