Na Bakari Lulela,Timesmajira
WAZAZI kote nchini wametakiwa kufuatilia mienendo ya vijana wao ili kuepuka vitendo hatarishi vya ushawishi,uovu ,uchochezi ambayo vimekuwa vikikithili siku hadi siku ndani ya Taifa letu
Akizungumza jijini Dar es salaam kwenye kongamano la amani, uchaguzi na malezi la wanawake wa Juakita (Bakwata) mgeni rasmi ambaye amesema kuwa mshauri wa Rais wanawake na makundi maalumu Bi Sofia Mjema alisema kuwa wazazi / walezi hakikisheni mnawafuatilia mienendo ya vijana wenu kwenye makundi yao.
“Hivi sasa Kuna mambo kemkem yanayohusu teknolojia ambapo vijana wetu ndio kimbilio lao hivyo tuwe makini katika kufuatilia masuala hayo kwa mabaya kuyakemea ambapo huharibu taswira njema na kuchochea mambo mabaya ya kuvuruga amani ya nchi yetu,” amesema Mjema
Aidha Mjema alisema kuwa nchi yetu inakaribia kufanyika kwa uchaguzi mkuu hivyo ni vema kumsemea mazuri Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassani kwenye mambo mbalimbali ambayo aliyokuwa amefanya katika kuiletea nchi hii maendeleo .
Aliendelea kusema kuwa miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya Barabara, madaraja, ujenzi wa mashule ,Reli ya kisasa na program ya M mama iliyoanzishwa kwa dhumuni la kuwasaidia akinana vipindi vya kujifungua.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Jua kita mkoa wa Dar es salaam Bi Mariamu Mtambo alisema kuwa akina mama mnatakiwa kuwa mabalozi wazuri katika kulinda na kudumisha amani ambayo ndio tunu ya Taifa letu na nyinyi ndio majemedari wakubwa hapa ulimwenguni.
Hata hivyo amani, utulivu, usikivu ni vitu muhimu katika ujenzi wa nchi yetu ambapo hujenga taswira bora na chanya katika kuleta maendeleo kwa jamii ya kitanzania.
Nae Mufti wa mkoa wa Dar es salaam Shekh Ally Ngeruko alisema kuwa vijana wetu ndio msingi wa maendeleo ambapo wengi ndio walioshika madaraka serikalini hivyo wanatakiwa kujifunza mambo mengi kwa wazee ambao wanaelewa kwa Mapana chanzo cha harakati za uhuru na changamoto mbalimbali walizozipata vipindi vya ukombozi wa nchi hii.
Amesema wazee waliopigania uhuru wa Taifa hili kutoka kwenye mikono ya wakoloni wanajua mengi dhidi ya changamoto mbalimbali walizozipata katika kumuondoa mkoloni hadi ukapatikana uhuru.
Kongamano hilo lilihudhuliwa na mamia ya wakazi wa Dar es salaam na wengine kutoka pembezoni mwa mji huo na baadhi ya taasisi ikiwemo Jai mat, wanawake na Samia, Wanawake na Juikita ,Yamka vikoba Tanzania, Juvikiba pamoja na chama cha watu wenye Ulemavu.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi