April 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wawekezaji watakiwa kuwekeza kwa tija

Na Mary Margwe, Timesmajira Simanjiro

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amewataka wawekezaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kuhakikisha uwekezaji wao unakua na tija kwa wananchi,ili kukabiliana na changamoto za maeneo husika na si vinginevyo.

Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Sukuro Kata ya Komolo Wilayani Simanjiro,Sendiga,amesema wawekezaji waingie kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu zilizoweka na Serikali huku akionya kuwa wakiingia kimya kimya atawatafsri vingine.

Sendiga amesema Wilaya ya Simanjiro ndio inayoongoza kuwa na wawekezaji wengi kuliko Wilaya zote za Mkoa wa Manyara,na wananchi wake wana changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara, maji huku wawekezaji wakiwa wametulia wakiendekea kufanya yao.

“Licha ya uwepo wa wawekezaji wengi lakini bado changamoto nyingi zimeendelea kuwaelemea wananchi,kuonekana kwao hadi watakapokua wamegombana huko ndio utasikia kumbe Kijiji hiki kulikua na wawekezaji kadhaa.Wakishakutana na Serikali za vijiji baadhi ya Viongozi ambao sio waaminifu wanapatana nao hutowajua wala kuwasikia,”.

Hivyo amemtaka Mkuu wa Wilaya hiyo Fakii Lulandala, kuhakikisha anampatia orodha ya wawekezaji wote waliopo katika Halmashauri hiyo,huku akisisitiza kuwa Mwekezaji yoyote anatakiwa kujitambulisha kwenye Serikali ya Wilaya.

“Lengo ni kujua anayewekeza katika Kijiji hiki ama kile ni nani, je wananchi wanamtambua, anaisaidiaje jamii inayomzunguka pale.Tuone uwekezaji wake ni halali lakini,unatija kwa jamii husika,tumepata bahati ya ardhi ambayo imebeba mali nyingi chini, lakini wanaoweza wahusika wasinufaike ila wao,”.

Hata hivyo amesema ifike mahali wawekezaji watambue wajibu wao kwa wananchi,barabara ikibomoka wanasubilia Serikali ipeleke fedha ya kuichonga wakati matoli yao yanapita muda wote,hivyo amesisitiza kuwa itakua ngumu kuendelea na Mwekezaji asiye na faida