Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Imeelezwa kuwa upigaji kura ni haki ya msingiĀ ya kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea,hivyo wito umetolewa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 29,2025.
Wito huo umetolewa Septemba 28,2025 na baadhi ya wavuvi wa Mwalo wa Igombe uliopo Kata ya Bugogwa wilayani Ilemela mkoani Mwanza, baada ya kupatiwa elimu ya mpiga kura iliotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC), kupitia ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ilemela,iliotolewa mwaloni hapo.

Mbali na elimu ya mpiga kura pia walielimishwa juu ya taratibu za upigaji kura, umuhimu wa kampeni na maboresho ya sheria yaliyofanywa na INEC.
Mmoja wa wavuvi wa samaki katika Mwalo wa Igombe,Peter Bukana wamesema upigaji kura ndiyo njia ya kupata kiongozi wanayemtaka.hivyo.amewahimiza wananchi wenzake kujitokeza kupiga kura,kwani vituo vitakuwa wazi kuanzia saa 1 asubuhi hadi 10 jioni.
Kwa upande wake Ofisa Uchaguzi wa Jimbo la Ilemela, Shilinde Malyagili, amesisitiza kuwa INEC imefanya maboresho katika sheria ya uchaguzi ikiwemo kuruhusu mwananchi kupiga kura ya kuchagua Rais hata kama yupo nje ya kituo alichojiandikisha, kwa kufanya maombi mtandaoni au kujaza fomu maalum.
Ikumbukwe kuwa Septemba 15, 2025, Tume ilitoa tangazo la kuruhusu wananchi waliopo maeneo tofauti kutuma maombi ya kupiga kura ya Rais ambapo zoezi lilianza Septemba 19,2025 hadi Oktoba 2, 2025.

Shilinde amesema, tayari watu zaidi ya 20 kutoka Igombe wameishajaza fomu hizo huku akisisitiza kuwa baada ya zoezi hilo Msimamizi wa Uchaguzi huziingiza kwenye mfumo na mpiga kura hupokea ujumbe mfupi wa simu kuthibitisha.
“Tume ikishakubali, mpiga kura atapata taarifa rasmi na siku ya uchaguzi ataweza kupiga kura katika kituo alichoomba,ā amesema Shilinde.

More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi