January 27, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wavuvi 540 waokolewa Ziwa Rukwa

Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online,Rukwa

Wavuvi 540 waliokuwaa wanafanya shughuli za uvuvi ndani ya Ziwa Rukwa,wameokolewa huku 10 wakiendelea kutafutwa.Tukio hilo limetokea Januari 23,2025, baada ya upepo mkali uliotokea kwenye ziwa hilo, wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.

Kufuatia tukio hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa,amefika Kata ya Nankanga na kuungana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji, kujionea kazi ya uokozi huku akiwa ameambata na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF John Masunga pamoja na Askari Wazamiaji.

Akitoa taarifa ya tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbwanga,Nyakia Chirukile,amesema Januari 23 ,2025,wavuvi hao kutoka Kata ya Nanganga na Mtowisa, waliokuwa wanaendelea na shughuli za uvuvi ndani ya ziwa Rukwa walipatwa na dhoruba ya upepo mkali.

Ameeleza kuwa jitihada za kuokoa zinazoendelea kufanywa na Wananchi wakishirikiana na Jeshi la Zimamoto wa Uokoji , na hadi kufikia Januari 24,2025 saa moja usiku,wavuvi 10 walikuwa bado hawajapatikana

Akitoa salama za pole, Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa,amesema kuwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kupata taarifa hizo, ametoa helkopta ya Jeshi iliyoambatana na wazamiaji na vifaa maalum vya uokozi ili kuongeza nguvu za uokoaji

Kwa Upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvu,Dkt.Ashatu Kijaji, ametoa pongezi kwa wananchi kwa kushiriki kikamkalifu katika uokoaji pamoja na kutoa ushirikiano wa kuwatambua wavuvi wengine ambao walikuwa hawajasajiliwa katika vikundi na kampuni.