Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online,Nkasi
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi,wamesisitizwa upendo pamoja na kufanya kazi kwa weledi ilikuleta ufanisi wenye tija kwa Wananchi.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Nkasi,Afraha Hassan,Novemba 15,2024,wakati akisikiliza kero za watumishi wa Halmashauri hiyo,ambapo alizipatia ufumbuzi .
Sanjari na hayo amewataka watumishi hao kufuata sheria ,kanuni na taratibu za kazi pindi wanapotimiza majukumu yao Huku akiahidi kushughulikia changamoto na kero za watumishi pindi zinapojitokeza.
Aidha amewasisitiza na kuwashauri watumishi hao, kuachana na tabia ya majungu na kusemana na badala yake wajishughulishe na fursa mbalimbali ambazo zinapatikana katika Hamashauri hiyo ili kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi,Raineli Mwenda, amewakumbusha watumishi kuzingatia sheria kanuni taratibu za kazi.Pia kuwa na nidhamu ya kazi pindi wanapotimiza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuwahi na kutoka kazini kwa muda uliopangwa.
Pia ametoa rai kwa watumishi wa Halmashauri ya Nkasi,kuendelea kujifunza kwa bidii mfumo wa PEPMIS,ambapo zoezi la kuingiza malengo katika mfumo bado linaendelea,ambapo amewataka zoezi hilo likamilike kwa wakati.
More Stories
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25