January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

watumishi wa umma watakiwa kutumia mifumo ya serikali kwa weledi

Na Israel Mwaisaka,Timesmajira Online,Rukwa

Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Damas Makweba amewataka watumishi wa umma mkoani Rukwa kutumia mfumo wa ununuzi wa elekroniki (NeST) kwa udailifu ,uwazi na uwajibikaji ili kufikia malengo ya serikali.

Ameyasema hayo kupitia kikao kazi kilicho jumuisha watumishi wa umma wilayani Kalambo mkoani Rukwa ,ambapo amesema mfumo huo umelenga kurahisisha upatikanaji wa thamani ya fedha katika ununuzi na ugavi pamoja na ufuatiliaji wa sheria za ununuzi kwenye taasisi za umma.

Makweba amefafanua kuwa suala la ununuzi linahitaji uadilifu ili kuepusha migongano baina ya mnunuzi na serikali,uwazi na uwajibikaji, thamani inayolingana na ubora pamoja na zabuni za uwazi na ushindani.

‘’Wateja wanaweza kufanya manunuzi popote walipo na wakati wowote bila kuhitaji kwenda dukani,NeST pia hutoa usalama wa malipo na inalinda taarifa za kibenki za wateja, hivyo kufanya manunuzi kuwa salama zaidi,”amesema Makweba

Aidha amesema matumizi ya NeST yamekuwa na mafanikio makubwa kwani kampuni nyingi zimekuwa zikitumia mfumo huo kwa kufanya biashara zao kwa ufanisi zaidi na kuvutia wateja wengi Zaidi.