November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watumishi wa Fahari wafanya Bonanza

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

WATUMISHI Walimu wa Shule ya English Medium Fahari Elite ,Iliyopo Kiboga wilayani Ilala, wamefanya Bonanza la shule hiyo kwa kushirikisha shule za Mvuti kwa lengo kujenga afya na mahusiano.

Akizungumza katika Bonanza hilo Mkurugenzi wa shule ya Fahari Elite Neema Mchau, alisema Fahari Tuamke Maendeleo kila mwaka wamepanga siku maalum Watumishi wa shule hiyo kwa kushirikiana na shule za jirani kwa ajili ya Bonanza la shule.

“Bonanza letu ni endelevu tunafanya kila mwaka katika shule zetu za fahari napongeza Wajumbe wa Kamati za shule kwa kufanya Bonanza hili na watumishi ambapo michezo mbalimbali leo imefanyika “alisema Neema.

Neema Mchau alisema katika Bonanza hilo wameshirikisha Michezo ya kuvuta kamba ,Kuvuta magunia,Rede,mpira wa miguu Wanawake na Wanaume, kukimbiza kuku,Kukimbia na mayai .

Alisema katika michezo hiyo Washiriki Walimu,wa Fahari, Watumishi wasio Walimu na Wanafunzi na shule za jirani zote za Mvuti .

Shule ya Fahari Elite English Medium iliyopo Chanika Kiboga ya kisasa inapokea wanafunzi wa elimu ya msingi na darasa la awali ina walimu wa kisasa madhari nzuri
Mkurugenzi wake mgeni rasmi , Christopher Chinyara ,aliwataka walimu na Wanafunzi kufanya michezo kila wakati kwa ajili ya kujenga afya na mahusiano mazuri.

Chinyara alisema shule ya Fahari wanaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kukuza sekta ya michezo iweze kukua.